ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, September 5, 2013

Mama wa Dillish kazungumza kuhusu mwanaume aliedai ni baba Dillish



Siku moja iliyopita Jarida la Pulse Kenya lilitoa taarifa ya mtu anaitwa Abdi kujitokeza na kusema yeye ndio Baba mzazi wa mshindi wa shindano la Big Brother The Chase 2013 Dillish wa Namibia.

Abdi ambae asili yake ni Somalia alitoa taarifa hiyo nchini Kenya ambako anadai kuwa alizaa na mwanamke wa Kinamibia wakati alipokwenda nchini humo mwaka 1989 akiwa mwanajeshi wa jeshi la kutunza amani.

Taarifa hizo zilikutana na hisia mchanganyiko huku wengi wakiwa wanasema baba huyo amejitokeza kwa kuwa mtoto amepata umaarufu na utajiri wa fedha alizoshinda kwenye shindano la BBA lakini Dillish mwenyewe hakuwa na hisia nzuri kuhusiana na taarifa hizo.

Mrembo huyo kupitia page yake ya Twitter alihoji hivi “Nasikia eti baba yangu ni Msomali, alianguka toka wapi” . Mrembo huyo alionekana kuungana na wale waliosema kuwa mzee huyo ni mwongo ambapo aliretweet mawazo yao.
Inasemekana kuwa hakuna mtu anayeweza kumfahamu vizuri baba yako kama mama yako mzazi na mama yake Dillish anaonekana kumfahamu mtu huyo anayedai kuwa ni Baba mzazi wa Dilish, Mama huyo ( Selma Pashukeni ) akiwa na viongozi wa ubalozi wa Kenya huko Namibia alionekana kujawa na furaha baada ya kuunganishwa na Abdi anayedai kuwa mpenzi wake wa zamani na walizungumza kwa mara ya kwanza baada ya miaka 23.

Selma alionekana kujawa na hisia kali baada ya kumuona Abdi na wawili hao walijawa na furaha wakati wakizungumza na mama huyo hakuonekana kuwa na hasira au chuki yoyote dhidi ya Abdi na mara moja walianza kukumbushana maisha yao ya zamani walipokutana Namibia.

Selma alifikia hatua ya kumhoji Abdi juu ya wenzie aliokuwa nao wakati huo na Abdi alijawa na majonzi wakati akimwambia kuwa wamefariki dunia.

No comments: