Patrick Naggi
Wakati kamati ya utendaji ya klabu ya Yanga ilitarajiwa kukutana jana jioni katika kikao cha dharura kumjadili Mkenya anayedaiwa kuwa katibu mkuu mpya wa klabu hiyo, Patrick Naggi, habari zilizopatikana jana zilidai kuwa Mkenya huyo hakuwa na baraka yoyote ya wajumbe wa kamati hiyo.
Baada ya vuguvugu la wazee wa Yanga lililotokea klabuni juzi, jana Naggi hakufika kwenye makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo kwenye makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar es Salaam kama ilivyokuwa kwa siku tatu zilizopita.
Akizungumza na NIPASHE jana, mmoja wa wajumbe wa kamati ya utendaji (jina tunalo) alijitolea mfano yeye, akisema kwamba hakuwahi kuitwa au kushiriki katika mazungumzo yoyote yanayohusu mchakato wa kumpata katibu huyo kutoka Kenya.
Mjumbe huyo alisema kwamba yeye na wenzake kadhaa hawapingi klabu yao kuajiri katibu kutoka nje ya nchi lakini ni lazima taratibu za kawaida za kumpata mtendaji huyo mkuu zifuatwe kama katiba yao inavyoelekeza.
"Kwakweli mimi sikuwa na taarifa yoyote kuhusiana na uteuzi huo… na leo (jana) jioni tumeambiwa kuna kikao na ajenda haijasemwa, ila ni wazi suala hilo litajadiliwa kutokana na hali ilivyo sasa," alisema mjumbe huyo.
Aliongeza kuwa kikao hicho kilitarajiwa kuangalia zaidi utaratibu uliotumika kumpata mtendaji huyo na wataangalia zaidi maamuzi ya kujenga kwani wanataka timu yao ifanye vizuri na kutetea ubingwa wake.
Makamu mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, alikiri jana kuwa ni kweli hakuna kikao chochote cha kamati ya utendaji kilichokaa kujadili uteuzi mpya wa nafasi hiyo muhimu katika klabu yao inayoshikilia ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Hata hivyo, aliongeza kuwa uongozi uliipa kazi kampuni moja (hakuitaja jina) kuendesha mchakato wa kupata mtendaji mkuu wa klabu na Naggi ndiye aliyeonekana mwenye uwezo kuliko waombaji wengine waliojitokeza.
Aliongeza kuwa baada ya Naggi kupitishwa na kamati ndogo waliyoiteua hakuwa amepewa barua ya kumfahamisha cheo chake rasmi ndani ya Yanga baada ya kuwasili nchini.
Aliyekuwa kaimu katibu mkuu, Lawrence Mwalusako, aliiambia NIPASHE mapema wiki hii kwamba amemaliza mkataba wa mwaka mmoja aliopewa tangu Septemba mwaka jana na kwamba hakuongezewa mkataba mpya.
Naggi akiwa kwao Kenya, aliwahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi baadhi ikiwa ni ya Mkurugenzi wa Ufundi wa Kampuni ya Ligi ya Soka ya Kenya (FKL), Afisa Mtendaji Mkuu wa timu ya Tusker, kocha mkuu wa klabu ya Nzoia, timu meneja wa AFC Leopards zote zinazoshiriki Ligi Kuu ya Kenya na vile vile kuichezea timu ya soka ya Akati iliyokuwa inashiriki Ligi Kuu ya Kenya na timu ya Taifa ya Kenya (Harambee Stars).

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment