Rais Macky Sall wa Senegal amemteua mwanamke kuwa waziri mkuu mpya, masaa tu baada ya kumtoa kazini mwanasiasa aliyemteua aliposhika madaraka mwaka jana.
Aminata Touré, waziri wa zamani wa sheria, aliiambia redio ya taifa kwamba amekubali amri ya rais ya kuunda serikali mpya.
Haikutolewa sababu ya Bwana Adbou Mbaye kutolewa kazini.
Bwana Mbaye, aliyewahi kufanya kazi kwenye benki, hakuwa mfuasi wa chama chochote cha kisiasa.
Bi Touré atakuwa mwanamke wa pili kuwa waziri mkuu nchini Senegal - baada ya Madior Boye, aliyeshika wadhifa huo kwa miezi 18 mwaka wa 2001.
Bwana Sall alimshinda Rais Abdoulaye Wade katika uchaguzi wa rais wa March 2012, akiahidi kupambana na umaskini na rushwa. )
No comments:
Post a Comment