ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, September 8, 2013

Picha ya Mheshimiwa Mbilinyi akipigana Bungeni inazungumza mara milioni moja zaidi ya maneno

MOHAMED MATOPE
Kwenye kampeni ya uchaguzi wa  raisi wa Amerika mwaka 1988 kulikuwa na mgombea mmoja anayeitwa Senator Gary Hart .Senator Hart wa steti ya Kolorado,  alikuwa  kijana anayevutia sana,mtu mwenye akili kupita kiasi ,mwanasheria aliyebobea na aliyeitumikia  serikali kwenye nyadhifa nyingi. Senator Hart alikuwa anaongoza kwanye kura za maoni kabla picha yake haijatolewa kwenye gazeti akiwa amekaliwa mapajani na mrembo (model) Donna Rice,ambaye alikuwa ni kimada wake.Ilichukua usiku mmoja kwa Senator Hart,kuporomoka kwenye kura za maoni ,kutoka asilimia thelasini na mbili mpaka asilimia kumi na saba.

Picha ya mgombea mweshmiwa Mheshimiwa Joseph Mbilinyi (Sugu),iliyotolewa magezitini akiwa amenyanyuliwa miguu juu,  na askari wa bungeni inamadhala sawa na ya Senator Gary Hart.Muheshimiwa Mbilinyi sio kiongozi wa upinzani,na pengine hatokuwa mgombea wa uraisi wa upinzani, hiyo inaelewaka dhahiri.Lakini jambo kubwa ni kwamba, Mh. Mbilinyi ni mbuge wa upinzani,kwa hiyo jambo lolote anolofanya , zuri au baya linaathili upinzani wote nchini.

Naelewa sio fair kwa kosa la kiongozi mmoja wa upinzani, liwaathili wapinzani wote,lakini ,binadamu ndio tulivyoumbwa ,tunajaji jumuia yote kwa kosa la mwanajumia mmoja.Na kwenye  siasa  kukumbanisha wapinzani wako pamoja ni mchezo wa kawaida.

Picha ya Muheshimiwa Mbilinyi ,italeta madhala makubwa mawili kwenye upinzani.Lakwanza, ni imevunja IMANI ndogo wanachi waliokuwa nayo kwenye upinzani.Ukiangalia uchaguzi wa uraisi wa mwaka 2000,2005 na 2010 ,wanachi wengi waliipigia kura  CCM, kwasababu ni chama ambacho wanakifahamu, kimewaongoza kwa muda mrefu,ndio,hawana raha nacho sana, lakini wanakiamini kwasababu wanakielewa.

Ni sawa na kuendeshwa baharini na kapteni wa meli ambaye amekuaendesha wewe na familia yako miaka zaidi ya hamsini,bila ya kukuzamisha baharini na kukuua. Unapoamua kumuajiri kapteni mpya jambo la kwanza utataka kufanya ni kumuelewa huyo kapteni mpya ili ujenge uaminifu juu yake.Picha ya mheshimiwa mbilinyi itawafanya wananchi wajiulize mara mbili,je tanawaamini wapinzani kutosha kuwakabidhi usukani  wa meli watuendeshe baharini kwa miaka mitano bila kutuzamisha?

kama leo wanapigana wakiwa ndani ya Bunge , je tukiwapa uraisi si watauwana ndani ya Ikulu

Jambo la pili picha ya Muheshimiwa Mbilinyi ilichofanya ni ,imewalaisishia kazi CCM kwenye kampeni ya 2015. Imewapatia CCM advertisement ya bure. Kama CCM wataitumia hii picha  ya Muheshiwa Mbilinyi kiuharisi ,na kuionyesha  katika kila kona ya nchi, kwanye TV,matangazo na mabango ,na kuwauliza wananchi  swali moja tu ,ndio hata kama mmechoka na sisi, hata kama hamtupendi, je mpo tayari kuwakabidhi serikali yenu tukufu  watu kama  hawa? Na kama CCM wataweza kumuunganisha Mh. Mbilinyi na wapinzani wote kwenye boxi moja, case closed! Uchaguzi utakuwa umeisha.

Mwalimu Nyerere alituhusia kuwa Ikulu ni mahari patakatifu,na kama Ikulu  ni mahari patakatifu,basi utakatifu unaanzia bungeni. Maraiisi wetu wote waliotawala nchi yetu wametokea bungeni.Vile vile,bunge linatunga sheria za nchi,na watanzania wengi leo wanatumikia vifungo kwenye majela kwasababu wamevunja sheria zilizotungwa  na bunge,kwasababu hiyo, tunawashikilia wabunge wetu kwenye standadi ya juu.

Senator Hart, alitumia wiki nzima kujielezea ,na kuomba misamaha ya kila aina,lakini haikusaidia, mwishowake akaliondoa jina lake kwenye kugombea uraisi.Labda Muheshimiwa Mbilinyi anao ufafanuzi mzuri wa mambo yaliyotokea bungeni kabda hajanyanyuliwa kichwa chini miguu juu na polisi wa bunge,na pengine hakuvunja sheria yeyote ya nchi.Naibu Spika alishamsamehe,na amemruhusu kurudi bungeni ,hana sababu yeyote ya kujiuzuru kama senator Hart, lakini  (damage is done ) picha inazungumza mara milioni moja zaidi ya maneno.
 Mwisho.

Mohamed Matope ni mwandishi wa blogu mbalimbali za Tanzania na Afrika.

30 comments:

Anonymous said...

hiyo picha haiwezi kuwaharibia upinzani wala mh mbilinyi kwasababu Mh Mbilinyi yeye ndio kaanza kupigwa na kubebwa juujuu.ulitaka afanyaje?pili imeonyesha naibu spika wa alivyokosa busara na yeye ndie anaepwashwa kulaumiwa.kwakiongozi mwenye busara huwezi kumuamrisha mbunge mwenzako kama mtoto kaa chini.hii picha imeonyesha jinsi chadema walivyokuwa tayari kupigania haki zao zakimsingi bungeni na imeonyesha ccm ilivyokuwa tayari kwa lolote hata kuua kulinda maslah yao...bwana Mohamed pamoja nakwamba wewe ni ccm lakini jaribu kuwa mkweli kwa maslah ya umma kumbuka wewe ni muislam kesho kunamwanandani anakusubiri ukiwa peke yako.usijaribu kupotosha umma kwa manufaa ya wachache

Anonymous said...

hii picha
inaonyesha police brutality

Anonymous said...

CCM imezeeka na inafanya mambo ya aibu mengi na yakipuuzi na ya ovyo Tanzania,kaka huo mfano ulioutoa wa seneta wa marekani...Tanzania sio marekani na vyama vingi wanawapinga ccm kwa sera zao za kipuuzi na uwizi ,ufisadi,...nchi haina maendelea so unapompinga mtu unatumia njia yeyote ile!sikia kaka matope!amani ,utulivu haviwezi kuwepo mpaka haki iwe imetangulia!!CCM iliyokuwa kipindi cha mw.nyerere sio ya sasa ...sasa hivi ni Chama cha matapeli..unapokuwa mwana siasa unakubali Aibu pia kwa masilahi ya baadae na kuondoa woga kwa wanasiasa wanaokuja ...MPIGANAJI

Anonymous said...

Bwana Matope mimi ni kati ya wachache ambao wanaopenda nukuu zako katika blog hii ya vijimambo. Nimekuwa nikisoma kuanzia zile za shauku juu ya mama majaa, mpaka ya mwisho ya Treyvon Martin. Mimi ni CCM wa kizazi kipya (Vijana tunaotoa muona wa kweli bila kujali itikadi au fikra fukara za kizamani)
Mapenzi ya kibubusa na ufinyu wa mawazo ndio uliotukwamisha katika maendeleo ya mambo mengi tu muhimu, ndio maana hata katika CCM tunamikakati ya kuwapumzisha wazee wetu katika nafasi za juu za utungaji sharia na utawala na kuwaingiza vijana kupata fikra mpya zilizoshiba haki na ukweli.
Sasa wanapotokea vijana, wanaofanana na mimi na kutoa mitazamo mibovu na potofu, umrudishi nyuma Matope, bali vijana wa CCM, unatufanya sote sisi kuwa hatuna uwazi wala fikra bora kwa kukiongoza chama chetu.
Ningependa ifahamike kwako na kwa wote wanaotaka kuzungumza kwa niaba ya CCM, CCM yetu ya leo ni ya wazi na yenye mitazamo yenye siha. CCM ya leo tunakemea upotovu na kusimamia haki bila kujali nani kaongea na katoka chama gani.

Suala la kumbeba Mh.Mbilinyi ni la kihuni na CCM linakemea suala hili. Tunaamini heshima ya hali ya juu kwa wabunge wote bila kujali vyama vyao. Tutaendelea kupingana kwa hoja, kutoleana maneno makali na hata kunyoosheana vidole, ndio katika jitihada za kutumikia jamii zetu na ari za ushindani zilivyo. Demokrasia ya uhuru wa kushindana, kutofautiana na kuwa na ari ya uhuru wa kujikita na mtazamo imeletwa na CCM, na CCM itaendelea kuilinda.
CCM haihusiki na wala haikufurahishwa na uhuni huu. CCM ni chama kinachoongoza Serikali ya haki kwa jamii zote na watu wa aina zote.
Pamoja na kuwa kila mtu ana haki ya kueleza mtazamo wake, lakini si kila mtu anahaki ya kupotosha mtazamo wa CCM.
Bwana Matope, ukisoma nyumba ya kadi zetu za CCM kwenye Imani ya chama,zinasema;Binaadamu wote ni sawa. Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.
Kwa kambi ya upinzani,chadema,na vijana wasio na fikra huru tunapenda mtambue kuwa, CCM ni wastahamilivu na itaendelea kustahamili kosoro zozote ambazo zinatokana na ufujaji wa uhuru wa kujieleza. Pia tunapenda mfahamu kuwa pamoja na kasoro zote zinazojitokeza kwa tiketi ya CCM, CCM itaendelea kusimamia haki na Uhuru wa kila Mtanzania.

Hii picha haionyeshi kama Mbunge Mbilinyi anapigana,yeye ndio amekamatwa na watu nane wakimlazimisha kutoka nje ya ukumbi wa bunge.Matope sio vizuri kuwadanganya watu wenye akili zao.Toa kwanza boriti nyumbani kwako kuliko kibanzi cha Seneta Gary Hart.

Anonymous said...

Ndugai na Bibi Makinda wameliharibu bunge kwa kuonyesha upendeleo wa wazi kwa wabunge wa chama cha mafisadi.Katiba mpya,Spika hatotoka chama chochote cha siasa,mtu huru.

Anonymous said...

Sidhani kama una macho ya kibinadamu...labda niulize, mimi naona Mh. Mbilinyi kashikwa mikono, mguu mmoja,na mwingine upo chini. Sasa CCM wataitumia hii picha wakiwambia watu kwamba aliyekuwa anampiga mwenzake ni huyo aliyeshikwa mikono yote na mguu mmoja? Hivi mmefika hatua ya kudhani watu hawana uwezo wa kufanya judgement? too bad.

Anonymous said...

mdau hapo juu unanidai laki mia

Anonymous said...

Mh Matope, mimi naitwa Waigama, siyo mpenzi wa Chadema wala CCM. Pamoja na heshima na imani niliyonayo juu yako, sikubaliani na comment yako Kuhusu Mh Mbilinyi au kambi nzima ya upinzani kwa sababu zifuatazo. Kwanza sijui kama uliiangalia ile video tokea MWANZO mpaka alivyo onekana vile ktk picha ambayo umeifanya msingi mzima wa article yako kwenye Vijimambo. Please revisit the whole video first before reaching any conclusion. Umetoa mfano wa senator Hart na model, ambayo ilipelekea aanguke kwenye public opinions, perhaps ikamkosesha uraisi. Alikosa urais kwasababu ya character yake mbovu. Senator Hart hakutendewa na mtu, ila sasa ukifuatilia ile video Mh Mbilinyi tokea mwanzo, utagundua kuwa alikuwa victim of nothing, but humiliation. In American Politics, voters tends to sympathies with a victim. Kuna mifano mingi sana, ila upo wa karibu ambao watanzania wengi wanaweza kuuhusisha. Obama vs Clinton's machine in N Corolina is most recent example. Clinton's played race card--remember? Guess who won, bro? Obama, a victim of racism. Contrary to Matope's views, Mbilinyi was a victim here, and he deserves less scrutniny.

unanimous said...

ukinywa maji ya Bendera ya CCM....lazima uwe kipofu haingii akilini kuona picha ya juu na kuweka kichwa cha habari kuwa mbilinyi anapigana bungeni!..tunakubali kuwa Matope ni mkereketwa lakini hasijifanye mchambuzi WA maswala ya siasa kwa kupoteza ukweli ulio dhahiri

Anonymous said...

Matope hongera ulichosema ni sawa kabisa napenda akili yako

Anonymous said...

Yaani kuwacha chuki binafsi matope ameongea ukweli mtupu mbilinyi sio mwana siasa bali ni mu huni hakutakiwa kuwa mbunge kabisa aibu kubwa

Anonymous said...

Yule Mbunge wa CCM alietumia F word na huyu wa Mbunge wa Chadema. Je ni yupi alieshusha hadhi ya taifa.

Musituletee mambo ya Nyani haoni kundule.

Anonymous said...

Hee watu hebu tulieni muuangalie ukweli,hapa.Matope kaandika hii article bila kuukandia upinzani au kumlaumu Mr Mbilinyi.Yeye ameandika maoni yake.Hauwezi kumlaumu mtu kwa kutoa maoni yake.Let me put things in prospective here,nchi yetuhaijawahi kuona vurugu kama hii ndani ya bunge.Hatujui nini reaction ya wananchi.Labda wananchi watamuona Mh.Mbilinyi ni victim na wakaipongeza upinzani,au wananchi hawatopenda hii vurugu ndani ya bunge lao na wakamua kuupanish upinzani.Mr Matope katoa maoni yake tuu.Pili nampa hongera Matope kwa uwezo wake wa kifikira,hajamkashifu Mr Mbilinyi binafsi ,ameizungumzia picha na jinsi itakavyo viewed by wananchi.Mimi sina mengi lakini tumshukuru Matope kwa kuuleta huu mjadara.Tunahitaji kuona hivi vitu from different angle .Good article

Anonymous said...

Waatu,mimi ni independent lakini naelemea kwenye upinzani,lakini ukweli ni kitu cha bure.Hii picha haileti sura nzuri.sisi watanzania ni watu wa heshima,tunaweza kulumbana bila kupigana.Ugomvi ndani ya bunge ni mambo ya kizamani.Bungeni kuna taratibu zake na kama upinzani haulidhiki na sheria za bunge wanaweza kufuata taratibu zilizopo,sio kupigana.I hope viongozi wa upinzani watajitokeza kushutumu tabia hii ya kutokulieshimu Bunge letu.

Anonymous said...

Mr Matope hongera zako,meonyesha busara zako na analysis yako ni kubwa mno.Watu hawaelewi kitu kimoja,kama mbunge wa CCM akifanya kosa tunailaumu sio CCM tuu bali serikali nzima.Na kama mbunge wa NCCR akifanya kosa tunalaumu wapinzani wote.Hii ndio hali arisi.Lakini Matope umefanya kosa moja,umewapa wazo la bure CCM la kushinda uchaguzi wa 2015.Ulikuwa uwauzie hili wazo na slogani ya WANAPIGANA BUNGENI ,WATAUWANA IKULU.I wish we have many people with big brain like you ,kwenye chama.

Anonymous said...

Wape wape vidonge vyao hoooooooo.

Anonymous said...

Upinzani uabidi ujiangali sana,kama watu watawapersive kama ni wahuni basi hawatagusa Ikulu hat siku moja.

Anonymous said...

ukweli ni kwamba ,Mbilinyi sio mgombea wa uraisi,uinzani ukishindwauraisi itakuwa ni kwa sababu ya wananchi hawajawakubali.Nakubaliana na wewe kwamba watu wanaipigia kura CCM kwa sababu hawana choice lakini kama upinzani utajitokeza kama wana choice kwa watu wanabidi kwanza wajiheshimu.Mr Mbilinyi kachemsha ,hata kama ni mshabiki wake ,hii picha ni choo kitupu

Siasa mchezo mchafu sio chadema wala ccm hakuna wa kuleta maendeleo kwa wananchi,Tanzania itajengwa na watanzania wenyewe,ji ulize wabunge wangapi wameenda kijijini kwako wakasaidia ndugu zako? Kila siku kutaka sifa bungeni matusi,kashfa ndio zimetawala kwa wa bunge wa vyama vyote. Wapinzani jipangeni na sera zenu na CCM nao mjipange na wananchi angalieni chama gani kinawa faa na kimekuletea maaendeleo gani tangia mbunge wako awe madarakani msiburuzwe Kusoma hatujui hata kutazama picha nako huwezi? Soma alama za nyakati.

Anonymous said...

sikilizeni mwishon sugu wakati anampiga ngumi askar alitoa matusi''msenge ,ku..amenipiga huyu,
jamaa ni muhuni tu sio kiongozi. hawa watu hawafanani na mbowe kbsa

Anonymous said...

Mimi sio chadema au ccm lakini we mwandishi wa hii habari inaonyesha jinsi gani ulivyo na upeo mdogo wa ki fikra. Habari hii uliyoandika ni ya kichochezi na haina msingi haswa pale unapomfananisha huyu mbunge na yule senator wa Marekani "hahahaaaaa lmao" ningependa sana nikujue wewe ni mtu wa aina gani lakini kwa hii maandiko yako inaonyesha wewe ni mnafiki tu na huna hoja za msingi bali kupotosha watu.

Anonymous said...

Wamefuruga sana upinzani na pia n aibu sana kwa vitu kama hvo kutkea katka bunge letu tukufu

Anonymous said...

Kwanza Kiswahili kibovu! Jamani msipotishe lugha yetu! Una issue na 'L' na 'R' yaani umezitumia zisivyo na zinaharibu maana ya hii article.
Pili, hizi hadithi 2 hazina mahusiano na si sahihi kuanza article na hadithi ya Senator ambayo haina muelekeo na hili unalolizungumza.
Tatu, umepoteza maana ya article nzima sababu ya kutokuwa mkweli. Ukiangalia Video utaona wabunge wa Chadema walimzingira Mbowe ili asitolewe bungeni na polisi walivyoamrsiswa kumtoa Mbowe wakawatoa hao wabunge wa Chadema walioziba njia kwenda kumtoa Mbowe na mmojawapo ni Huyu Sugu na ndipo purukushani zikatokea na si sahihi kusema kuwa alipigana ndani ya bunge. Kilichotokea ni kukaidi amri ya naibu spika na kilichofuata ni kuondolewa kwa nguvu. LAKINI HAKUINUA MIKONO NA KUANZA KUPIGANA NDANI YA BUNGE.Alipokuwa nje ya bunge NDIPO ALIPOFANYA KITENDO CHA KIFEDHEHA CHA KUMPIGA POLISI. NASHUKURU KWA HUYO ALIYERECORD VIDEO MAANA UKIANGALIA VIDEO UTAJUA UKWELI UPO WAPI!
MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Anonymous said...

Huyu mtu aliyeandika hii comment ya juu, kwamba hii article haijapandilika ,na kukosoa kiswahili cha bwana Matope anachekesha sana.Yeye mwenyewe halichoandika hata hakieleweki.Amechanganya herufi kubwa na ndogo pamoja,hakuna panctuations.Pili huyu aliyeandika comments ni mtu ambaye labda kaishia darasa la saba au hajaisoma hii article ,how come haioni connection ya Senator Hart and Mbilinyi,connection yao kwenye hii article ni PICHA za embarassment ,na ndio kitovu cha article hii,Mr Matope ,mimi ni msomaji mkubwa wa article zako ,najua hii ni article yako ya kwanza kuandika kwa kiswahili ,umeipatia sana ,na nakuomba uwe unatuandikia kwa kiswahili,kwani ukweli ni kwamba wabongo wengi English hakipandi na wewe mzee umebobea sana,ndio maanacomments zimekuwa nyingi kwenye article hii.Pili Upeo wako ndugu yangu ni wa kutisha ,hata hawa wapinzani wanaokupinga kwenye comments wanaelewa kwamba uko objective,haujamkosoa Mr Mbilinyi ,sema umezungumzia hii picha ndiyo itakayommaliza .thanks.

Anonymous said...

Ukweli wa hii video tuseme ukweli,Mbilinyi kachemsha,watu hawagombani bungeni watu wanarumbana bungeni.Na reaction ya watu hapa bongo especially wasomi ambao wanausapoti upinzani ni mbaya sana.hii action ya sugu imewaaibisha wanachama wengi wa upinzani.

Unknown said...

Nice
Yote ni kuwa na serikali isiyo na udhibiti ktk utawala.