ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, September 17, 2013

SHEKHE PONDA ISSA PONDA ANYIMWA DHAMANA

 Sheikh Ponda Akishuka kwenye basi la Magereza tayari kuingia Mahakamani Kusikiliza kesi yake inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Morogoro.Sheikh Ponda alishatikiwa katika Mahakama Hiyo akikabiliwa na Mashtaka Matatu Ambayo inadaiwa aliyatenda Mkoani Morogoro katika Mkutano Hadhara mwezi uliopita.Kesi hiyo imearishwa tena Mpaka Tarehe 01.10.2013.Mshitakiwa Amenyimwa Dhamana na Amerudishwa Rumande.
 Sheikh Ponda akiwa Chini ya Ulinzi Mkali wakati akiingia Mahakamani kusikiliza kesi yake inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Morogoro.
 Sheikh Issa Ponda akiingia Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa Morogoro leo kusikiliza kesi yake
 Wafusi wa Sheikh Ponda wakiwa wakiwa mahakamani leo kusikiliza kesi ya Kiongozi wao iliyokuwa imetajwa mahama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro.
Ulinzi Mkali ukiwa umeimarishwa Mahakamani leo wakati kesi hiyo ikiendelea.Picha kwa hisani ya MATUKIO NA MICHAPO BLOG

1 comment:

Anonymous said...

Hiviiii hao wanaojiita wafuasi hawana kazi za kufanya kabisa jamani???? Ndo maana Tanzania lime kuwa Taifa la MAJANGA!!!! Mtu Unaketi mahakamani nje masaaa na masaaa unafuatila kesi kitu ambacho utakisoma tu kwenye magazeti na hata kwenye television!!!!!!! Wengine nimeona wana mpaka watoto wadogo wamewaleta mahakamani kufuatilia kesi!!!!!! Tanzania aaaamkeni! Umasikini tunauleta wenyewe! ! Aibu! Aibu!