
PROF. ANNA TIBAIJUKA
Alizaliwa Oktoba 12, 1950 huko Kagabiro, wilayani Muleba, mkoani Kagera. Ni Mbunge Jimbo la Muleba Kusini mkoani Kagera kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kwa sasa ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa (UN-HABITAT) kuanzia Machi 2006 mpaka Novemba 2010. Ana watoto wanne.
ILI kutambua na kuthamini mchango wa wanawake katika maendeleo ya jamii yetu, Kampuni ya Global Publishers and General Enterprises Limited, inatoa tuzo kwa mwanamke ambaye katika maisha yake amefanya mambo mengi zaidi ambayo yameinufaisha jamii na kuboresha maisha ya watu. Wanawake hawa hapa chini ni wale waliopendekezwa kuwania tuzo hiyo ya “The Woman Of The Year”. Ili kuwajua wanawake hawa soma wasifu wao na kisha umchague mmoja wapo atakayejishindia tuzo hiyo.
Hadi kuteuliwa kwa cheo cha Umoja wa Mataifa alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Januari 2006.
Chini ya Rais Benjamin Mkapa, alikuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto pia alikuwa mbunge kupitia viti maalumu kwa wanawake.
Kabla ya kujiunga na siasa alifundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Ana shahada ya uzamili ambapo mwaka 1992 akaongeza cheti cha udaktari wa sheria kwenye Chuo Kikuu cha Konstanz (Ujerumani). Kabla ya kurejea Tanzania kufundisha. Ameolewa na Cleophas Migiro na wana watoto wawili wa kike.

Ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mama Klementina inayoendesha shule ya wasichana wanaotoka kwenye mazingira magumu ambao wanaandaliwa kuwa wajasiriamali na viongozi bora katika jamii.
Aliwahi kuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru Mkoani Kilimanjaro kwa miaka 22, kuanzia mwaka 1970 hadi 1992.
Amekuwa akishauri serikali kuhusu suala la wasichana wanaopata mimba wakiwa shuleni waweze kurejea kuendelea na masomo baada ya kujifungua. Pia amekuwa akitoa miongozo kwa serikali kuhusu kuboresha elimu na kurejesha baadhi ya masomo ili kuhakikisha shule inamiliki miradi yao. ANNA KILANGO MALECELA
Alizaliwa tarehe 9, Januari 1956, ni Mbunge wa jimbo la Same Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi. Aliwahi kuwa Mhasibu wa KLM Airline, Mhasibu Msaidizi wa Air Tanzania Corporation (ATC), Mdhibiti Fedha wa Gulf Air Corporation. Pia aliwahi kuwa Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Kisutu na Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kinondoni. Ni mke wa mwanasiasa mkongwe nchini, John Malecela.
ANNANILEA NKYA
Huyu ni mama jasiri, amejitokeza kupigania haki na usawa wa wanawake na watoto. Amepambana kukomesha ukeketaji, mimba za utotoni, ukatili wa kijinsia na hasa kuhakikisha vyombo vya habari vinaandika na kufichua madhambi yote ya kuwanyanyasa na kuwatesa wanawake na watoto.Mama Ananilea Nkya, alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) tangia 2001 hadi mwaka huu alipomaliza kipindi chake.
Mama huyu alianza kazi ya uandishi wa habari 1982 RadioTanzania na wakati anajiunga na TAMWA 2001, alikuwa amepanda hadi naibu mhariri ndani ya Redio Tanzania na kuendesha kipindi cha kutetea haki za wanawake –MWANGAZA.
NB. ANDIKA JINA LA MWANAMKE MMOJA TU KATI YA HAWA ENEO LA MAONI HAPO CHINI.
IMETOLEWA NA GLOBAL PUBLISHERS LTD
IMETOLEWA NA GLOBAL PUBLISHERS LTD



5 comments:
Mama Anna Tibaijuka
ANANILEA NKYA
ANANILEA NKYA
ANANILEA NKYA
ananilea nkya
Post a Comment