ANGALIA LIVE NEWS

Friday, September 6, 2013

ZANCANA INAVYOWAKWAMUA WANANCHI ZANZIBAR

 ZANCANA Jumuiya ya Wazanzibari waishio Canada katika mwezi wa August 2013 wametoa misaada mbalimbali ikiwemo kufutarisha katika mwezi wa ramadhan, msaada wa nguo, mabegi ya shule kwa wanafunzi wa Mwambeladu , uniform kwa wanafunzi wa Rahaleo, Vitabu wa dua, Tasbeh na vito vya thamani kwa madrasa na nguo za madaktari na wauguzi kwa Wizara ya Afya Zanzibar.

ZANCANA tunafahamu mahitaji haya hayakidhi mahitaji ya wengi, Wananchi wanaohitaji msaada bado ni wengi na Jumuiya hii haiwezi kufanya peke yake bila msaada wako kwa hiyo basi tunajua unajali na una upendo wa Wananchi wako sisi tumeanza kidogo tulichonacho, ukiangalia picha hizi utaona hawa Wananchi wachache walivyokua na nyuso za furaha kupata msaada huu mdogo kutoka ZANCANA. Kama wewe umetokea Zanzibar au kwa yeyote yule anayependa kusaidia Jumuiya hii anakaribishwa, vitu tunavyokusanya ni viatu kwa wanafunzi, mabegi ya shule na vitu vingine vinavyoweza tumiwa na Mwanachi na kuwezesha kusukuma maisha yake ya kila siku kwenda mbele. Tafadhali wasiliana na ZANCANA manager Bishara Al Masroori 647 866 4312
 Picha juu na chini ZANCANA ikifutarisha.
 ZANCANA ikitoa msaada wa nguo za madaktari na wauguzi wa Wizara ya afya Zanzaibar.
 Juu na chini ni ZANCANA ikitoa vitabu kwa madrasa
 Picha juu na chini ni ZINCANA ikitoa misaada ya Uniform na magegi ya shule za Mwembeladu na Raha leo
kwa picha zaidi bofya soma zaidi

6 comments:

Anonymous said...

MSAHALLAH ALLAH AKUBARIKINI DAIMA AMIN TUNATAKA KUOONA MIFANO KAMA HII MINGI KUSAIDIA JAMI ALLAH AKUBARIKINI SANA KWELI MMETOKA KATIKA MIFUPA YA WAZAZIWENU ALLAH AKUBARIKINI SANA AMIN

NY

Anonymous said...

MashAllah m.mungu awazidishie imaan

Anonymous said...

asalam aleykum sina lakusema ila asanteni sana mungu akupeni imani namoyo huo huo nainshaalla jumuiya yenu [yetu] itazidi kwenda mbele kwa uwezo wa allah kazi mnayo ifanya nikubwa na malipo yake mtayapata mazuri kwani kutowa sijambo lamchezona kuwacha yenu kwa ajili ya allah kuwasaidiya ndugu zetu huko zanzibar asanteni jumuiya ya zancana huko canada

Unknown said...

Hongera. Inshallah Mwenyezi Mungu awatie hamasa Wazanzibari kore ulimwenguni wasaidie kunyanyua maosha ya ndigu na wazee wetu. Keep it up
Ummu Shamte

Fatma Nawawi said...

Mwenye ezi Mungu aibariki zancana na kusonga mbele. Allah awape moyo huo huo wa zanzibar canadians. Kwani kujitolea inataka moyo, but kwa Allah bila ya shaka ujira ni mkubwa. Ama kwa hakika ndugu zetu wanahitaji na in shaa Allah atujaalie kama alivyosema bi Ummu hapo, wanzanzibar kote ulimwenguni kuwa na moyo mmoja kama huo. Hongereni kina Bishara, Suleiman, Zamil na wengineo hapo pichani kwa kuwacha yenu na familia zetu na kwenda kuwajibika. That was my dream, keep it up n Allah bless you , aamin

Anonymous said...

Good job...Mungu akupeni nguvu za kuendelea...Amin