Flaviana Matata akimkabidhi mwalimu mkuu msaidizi wa Shule ya Msingi ya Minazini,iliyopo Mwananyamala B, Fina Kiocho msaada wa madaftari,pen na pensel ambao utasaidia wanafunzi wasiona uwezo wanaosoma shuleni hapo.
Baadhi ya FMF Stationaries Project zikiwemo pen, penseli pamoja na madaftari makubwa na madogo ambayo yatakuwa yazalishwana Taasisi ya Flaviana Matata Foundations ambapo zaidi kutoa msaada pia kuna zitakazokuwa zinauzwa na pia Taasisi inakaribisha makampuni ambayo yanahitaji kutoa msaada wa vifaa vya shule kuwasiliana nao na nembo yao itawekwa kwenye vifaa hivyo
Flaviana Matata akiongea na wanafunzi wa shule ya Mnazini akiwaambia wasome kwa bidii kwani alimu ndio kila kitu na kuwakumbusha kwa wale watoto wakike ambao watafaulu na wazazi hawatakuwa na uwezo FMF itasaidia kuwasomesha baadhi yao .
wasanii pamoja na warembo mbalimbali walijitokeza kuunga mkono harakati hizo za Flaviana
Flaviana Matata akiwa sambamba na waliowahi kuvikwa taji la Miss Tanzania Nancy Sumari na Faraja Kokota na Miss Ilala Kisa Zimba
Mwanamuziki Ommy Dimpoz alipata wasaa wakusaini kitabu cha wageni cha shule ya Minazini.
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Flaviana Matata Foundation (FMF) inafanya kazi ya kuhamasisha, kuwezesha na kusaidia wasichana nchini kwa kuwaelimisha na kuwapa misingi ya kuwajenga kuwa kati ya watendaji wazuri wanaochangia katika shughuli za maendeleo ya jamii. Ili kufanikisha hayo, Flaviana Matata Foundation (FMF) inawadhamini wanafunzi wasichana kwa kuwalipia ada za shule, kuwanunulia sare za shule pamoja na misaada mingine mbali mbali yenye kumwezesha mwanafunzi kusoma vizuri kuanzia elimu ya msingi, upili na hatimaye kufikia kwenye taasisi mbali mbali za elimu ya juu.
Malengo makuu ya Flaviana Matata Foundation ni pamoja na:
i. Kusaidia kuongeza idadi ya watoto wa kike wanaojiunga katika ngazi mbali mbali za elimu.
ii. Kuhamasisha harakati za kutokomeza umasikini Tanzania kupitia miradi mbali mbali ya elimu.
iii. Kuhamasisha wasichana kujiendeleza kufikia elimu ya juu pamoja na elimu ya ufundi.
iv. Kuwasaidia wanawake kujikwamua kiuchumi kupitia shughuli za kijasiriamali.
Katika kufikia malengo hayo, Flaviana Matata Foundation inazindua mradi wake unaootambulika kama “FMF Stationeries Project” hapa Tanzania.
Mradi huu unahusisha uuzaji na usambazaji wa vifaa vya shule (madaftari, kalamu za wino, kalamu za risasi, rula, mikebe n.k.) kwa mashirika, taasisi mbalimbali na watu binafsi.
"Tunataraji kutumia mapato yatakayopatikana kutokana na mradi huu katika kulipia ada, kununua sare za shule pamoja gharama nyingine zinazohusiana na kuwapatia elimu bora watoto wote ambao wapo chini ya Flaviana Matata Foundation pamoja na kufanya miradi mingine ya maendeleo inayohusiana na elimu".
Kuhitimisha uzinduzi wa mradi huu, Flaviana Matata Foundation imeamua kuitembelea Shule ya Msingi Minazini iliyopo Mwananyamala wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam na kutoa msaada wa madaftari, kalamu za wino na kalamu za risasi kwa wanafunzi wenye uhitaji ikiwa ni ishara ya mwanzo wa utendaji wa Tasisi kuelekea kufikia malengo ya mradi.
FMF inaamini kwamba hii ni njia mojawapo ya kuwafikia Watanzania na kuwahamasisha kutoa misaada katika shughuli za kuendeleza elimu. Katika uzinduzi huu, Mwasisi wa taasisi ya Flaviana Matata Foundation,Flaviana Matata ameambatana na wanamuziki pamoja na vijana wengine mashuhuri nchini ambao ni vioo katika jamii yetu.
Dhumuni ni kuhamasiha vijana wengine kujitolea katika kusaidia shughuli zinazohusiana na maendeleo ya elimu na kupiga vita na kutokomeza umasikini.
No comments:
Post a Comment