ANGALIA LIVE NEWS

Monday, October 7, 2013

JENGO LA TTCL MAKAO MAKUU LILIPOKUWA LIKIWAKA MOTO LEO ASUBUHI


Jengo la TTCL, Makao makuu, EXTELECOMS limeungua moto kuanzia majira ya leo saa 12:00 asubuhi hadi saa 1:20. (Kwa saa za Tanzania)
Moto huo ulikuwa unawaka katika ghorofa ya sita ya jengo hilo na ulikuwa unawaka katika vyumba vitatu kwa mara moja.
Mwandishi wetu alifanikiwa kufika katika jengo hilo na kujionea mishe mishe za wafanyakazi wakiondoa magari yao na magari ya shirika hilo kongwe nchini.
Magari ya kikosi cha zimamamoto kutoka kikosi cha ukoaji cha Jiji la Dar es Salaam yaliwasili saa 12:20, lakini kulikuwa na ubishani kati ya wafanyakazi wa zima moto na wale wa TTCL, baada ya wafanyakazi wa Zimamoto kulaumu kuwa walienda pale siku kadhaa zilizopita kukagua jengo lakini walifukuzwa kama mbwa,

Licha ya Kikosi hicho kuwahi hawakuwa na maji yenye pressure na ngazi za nje kufika hadi ghorofani, hali iliyopelekea watu kutumia ngazi za ndani kuingia kwenye jengo hilo hali ambayo ni hatari kwa maisha yao.

Gari ya Ultimate Security walifika mnamo saa 12:30 na kwa ushirikiano moto uliweza kufanikiwa kuzimwa.

1 comment:

Anonymous said...

Poor Management...hicho ndicho kinachoendelea...sasa qaliensaje shambani bila jembe? TZ vipi jamani....hivi tuko karne ya ngapi bado?