ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, October 23, 2013

KANISA LAVAMIWA JIJINI MWANZA...MMOJA AUWAWA NA WENGINE WAWILI WAJERUHIWA VIBAYA



Mtu mmoja ameuawa na wengine watatu kujeruhiwa kufuatia shambulizi lililofanywa na kundi la watu wasiofahamika usiku wa kuamkia jana katika kanisa la Gilgal Christian Worship Centre lililopo eneo la Pasiansi wilaya ya Ilemela jijini Mwanza.
Tukio hilo lililotokea majira ya saa saba usiku linamtaja Elia Lunyamila (35) ambaye ni mlinzi na ni mwenyekiti wa vijana wa kanisa kuuawa akiwa amejumuika kwenye ibada na waumini wengine Alex Msakuzi na Tumsifu Pungu ambao hali zao zinatajwa kuwa taabani wakipatiwa matibabu Hospitali ya Rufaa Bugando Mwanza baada ya kujeruhiwa vibaya kwa kukatwakatwa mapanga sehemu mbalimbali za miili yao. 

Askofu wa kanisa hilo Eliabu Sentoz amelaani tukio hilo akilitaja kuwa ni la kinyama kwani limefanyika sehemu ya ibada akiwataka wananchi kuungana pamoja kulisaidia jeshi la polisi katika kutoa taarifa kuwabaini wahusika wa shambulio hilo na akaiomba serikali kuongeza nguvu kukabiriana na wahalifu hao.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza , Ernest Mangu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo mpaka sasa hakuna taarifa za kuibiwa kwa kitu chochote ndani ya kanisa, hali ambayo inalifanya tukio hilo kuwa na maswali mengi likihofiwa kufananishwa na yale ya uchomaji moto Makanisa.
Ndugu na majirani pamoja na waumini waliomfahamu marehemu Elia Lunyamila aliyeuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana wakiwa wamekusanyika nyumbani kwa marehemu kuomboleza

No comments: