ANGALIA LIVE NEWS

Monday, October 7, 2013

MABINTI WEUSI (WA KIAFRIKA) WANA MVUTO ZAIDI KULIKO WAZUNGU? SOMA HAPA UJIBIWE!!!

Pengine huwa unajiuliza kwamba kwanini mzungu akivaa bikini na kutembea ufukweni mwa bahari hakuna anae shituka wala kupiga kelele, lakini binti wa ki afrika akivaa bikini na kutembea ufukweni au kupiga picha utasikia maneno mengi ya kumsifia, au kumsema kwamba yuko uchi. 
Ajabu ni kwamba wale wale wanaompigia kelele binti wa kiafrika ndio wasioshituka wamuonapo binti wa kizungu. Je, unajua kinachosababisha utata huu?
Tatizo sio utamaduni, mila au mazoea. Ukweli ni kwamba wanaume wengi wa kiafrika huvutika zaidi wanapomuona binti wa kibantu kuliko mzungu
Hali hii inasababishwa na mazoea ya wanaume wengi wa ki afrika kuwa na mahusiano (sex) na wasichana wa kwao (wabantu) na hivyo kuufanya ubongo kuvutika zaidi na rangi au maumbile ya aina fulani. 

Ndio maana mwanaume anaejenga uhusiano na msichana mwembamba, si ajabu akatafuta msichana mwingine mwenye umbile linalofanana na hilo endapo kama ataachana na huyo aliyenae. 
Ukweli huu unaungwa mkono na wanasayansi walioendesha uchunguzi maalum kutaka kujua vikolombwezo vinavyo mvutia mwanamume.

Mamia ya wanaume waliofanyiwa uchunguzi wa picha za ubongo walionesha kupata msisimko zaidi katika hypothalamus (sehemu ya ubongo inayoshughulika na mahusiano/sex) kila walipo oneshwa picha za mwanamke wa asili yake hasa kama muhusika hajapata kuwa na uhusiano na mpenzi wa rangi au asili nyingine.

Hata hivyo tofauti ilijitokeza kwa wanaume waliooa wanawake wa asili/rangi tofauti. Hata hivyo wanasayansi hao walikubali pia kwamba sura na umbile la mwanamke lilisaidia kuongeza msisimko kwa namna tofauti.

1 comment:

Anonymous said...

asilimia kubwa ya watu wa dunia wanapendelea weupe na hata wakikosa weupe pepe basi light skinned, ndio tena dada zetu wanasumbuka kujipaka mikorogo, na kujichubua chubua ili wangare. bila kuufumbia jicho ni ukweli usiopingika sura ya kuvutia na rangi ndivyo vitu vyenye nguvu zaidi kwa uzuri wa mwanamke, maumbile na tabia zinafuatia. mwanamke ameumbwa kupendeza hivyo wanaume wengi wanapenda kuangalia vitu vinavyowavutia na kuwapa burdani ya roho na reception ndo uankutana nayo mwanzo kuliko kitu chengine, rangi tena hata nyumba yako unapendelea iwe na rangi ya kuvutia sisemi nyeusi ni mbaya nasema majority duniani chaguo lao ni light. I don't mean to offend anybody mimi mwenyewe ni mweusi wa mpingo lakini utafiti wangu nimegundua hayo niliyoyaeleza.