ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, October 6, 2013

MAHAFALI YA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA LUTHER BAGAMOYO YAFANA‏

Kaimu Mkurugenzi wa Shule ya wasichana ya Luther iliyopo Mapinga Bagamoyo, Anna Kiwelu akiongea wakati wa Mahafari ya kwanza ya shule hiyo. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Dawasa Mary Ngonyani, Kulia ni Mkurugenzi wa Shule hiyo Dk. Aumsuri Kiwelu. Mahafari hayo ya kwanza yamewajumuisha jumla ya wanafunzi 45 ambao wanategemea kufanya mitihani ya kidato cha Nne hivi karibuni.

Baadhi ya wanafunzii wa kitato cha Nne katika shule ya sekondari ya wasichana ya Luther iliyopo Mapinga Bagamoyo wakiwa katika mahafali yao ya kwanza tangu kuanzishwa kwa shule hiyo mwaka 2010. Jumla ya wanafunzi 45 walihitimu.
Mlezi wa wa wanafuzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Luther iliyopo Mapinga Bagamoyo, Constansia Masawe akiwasalimia wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo waliofika katika sherehe ya mahafali ya kwanza ya Kidato cha Nne kwa shule hiyo.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Wanafunzi wa Shule ya sekondari ya wasichana ya Luther iliyopo Mapinga Bagamoyo mkoa wa Pwani wakifurahia jambo wakati wa Mahafali yao ya kwanza ya kidato cha Nne yaliyofanyika shuleni hapo.

Mgeni rasmi wa mahafali ya kwanza ya Kidato cha Nne katika shule ya sekondari ya wasichana ya Luther iliyopo Mapinga Bagamoyo mkoa wa Pwani Mkurugenzi Rasilimali watu wa Dawasa Bi. Mary Ngonyani, akimkabidhi cheti Zainabu Chungu wakati wa mahafali hayo. Wanaoshuhudia (wa pili kutoka kushoto) ni Kaimu Mkurugenzi wa shule hiyo Anna Kiwelu na Kulia ni Mkurugenzi wa shule hiyo Dk. Aumsuri Kiwelu.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Luther wakivishana mashada wakati wa mahafali yao ya kwanza ya kidato cha Nne tangu kuanzishwa kwa shule hiyo.
Mgeni rasmi wa mahafali ya kwanza ya Kidato cha Nne katika shule ya sekondari ya wasichana ya Luther iliyopo Mapinga Bagamoyo mkoa wa Pwani Mkurugenzi Rasilimali watu wa Dawasa Bi. Mary Ngonyani, akimkabidhi cheti Anna Kiwali aliyefanya vizuri katika masomo ya Hisabati na Sayansi wakati wa mahafali ya kwanza ya Kidato cha Nne katika shule ya sekondari ya wasichana ya Luther. Wanaoshuhudia, kulia ni Mkurugenzi wa Shule hiyo Dk. Aumsuri Kiwelu na Mkuu wa shule hiyo Mtanga Gerson .
Mtaalamu wa maabara na mwalimu wa masomo ya Chemistry, Biology katika shule ya sekondari ya wasichana ya Luther Bw. Kalistus Mwendapole akimuonesha Mkurugenzi Rasmali Watu Mary Ngonyani, alipotembelea maabara ya shule hiyo.
Baadhi ya wanafunzi kati ya 45 wanaosoma kidato cha Nne katika shule ya sekondari ya wasichana ya Luther iliyopo Mapinga Bagamoyo Mkoa wa Pwani wakimkabidhi zawadi ya kumshukuru mwalimu wao Mkuu Mtanga Gerson wakati wa mahafali yao ya kwanza ya Kidato cha Nne tangu kuanzishwa kwa shule hiyo mwaka 2010. 
Protoko Ofisa wa Shule ya sekondari ya wasichana ya Luther iliyopo Mapinga Bagamoyo Mkoa wa Pwani, John Mwakilya akiwapa utaratibu baadhi ya wanafunzi wa kidato cha Nne katika mahafali ya kwanza ya Kidato cha Nne katika shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2010. Jumla ya wanafunzi 45 wa kidato cha Nne wanategemea kufanya mtihani wa taifa hivi karibu.

No comments: