ANGALIA LIVE NEWS

Friday, October 25, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWASILI MKOANI KIGOMA KUZINDUA KIVUKO KIPYA CHA MV MALAGALASI WILAYANI UVINZA LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Kigoma wakati walipokuwa wakimpokea kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo mchana. Makamu amewasili mkoani Kigoma leo kwa ajili ya kuzindua Kivuko kipya cha Malagalasi katika Wilaya ya Uvinza leo. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia burudani ya ngoma za asili kutoka kwa wakazi wa Mkoa wa Kigoma, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma jana mchana, kwa ajili ya kuzindua Kivuko kipya cha Mv Malagalasi leo katika Wilaya ya Uvinza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia burudani ya ngoma za asili na kumpongeza mmoja wa wasanii hao wakazi wa Mkoa wa Kigoma, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma jana mchana, kwa ajili ya kuzindua Kivuko kipya cha Mv Malagalasi leo katika Wilaya ya Uvinza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza baada ya kukabidhiwa ripoti ya Mkoa wa Kigoma jana mchana. Picha na OMR

No comments: