
Mariam Carey katika picha enzi ya uhai wake jana Alhamisi Oct 3, 2013 alileta kitim tim alipojaribu kugonga geti la Jengo jeupe kwa Obama na aliposimamishwa na Polisi wa Capitol alikataa kutii amri na kuamua kukimbia kwa gari alilokuwa akiendesha la Infiniti ya 2005 kuelekea upande wa Capitol Hill huku akufukuzwa na Polisi wa Capitol na kusababisha taharuki kwa Polisi na raia waliokuwepo maeneo ya tukio na baadae alipigwa risasi na kufa na mtoto wake kuchukuliwa na wanausalama.

Kizaizai mtaa wa Constitution gari la Polisi likiwa meng'emeng'e

Hapa ndipo alipouwawa Mariam Carey wakati alipokaidi amri ya Polisi walipotaka ashuke kwenye gari

Polisi aliyejeruhuwa akikimbizwa kwenye helkopta awaishwe hospitali.

Gari la Polisi kwa picha ya karibu.

DC palikuwa hapatoshi.

Ilikuwa mshike mshike.

Mariam Carey akibebwa kwenye machela kumuondoa sehemu ya tukio.

Polisi wa Jengo Jeupe akifuatilia tukio kwa karibu na darubini. (Picha kwa hisani ya ABC)
4 comments:
Akiwa muislamu anaitwa terrost, lakini akiwa siyo muislamu, anaitwa mgonjwa wa akili.
Sasa wewe anony wa 12:06 mbona unataka kuleta swala la udini sehemu ambayo aistahili.Je ulisikia huyo dada alikuwa amebeba silaha au alikuwa na bomu kama ma terrost wengine? Umesoma taarifa vizuri juu ya tukio hilo?Kuna ushahidi wa kutosha huyo dada alikuwa anamatatizo ya akili au unabisha na hilo?
jina lake Miriam sio Mariam!!
Samahani mdau, ila tumekuwa tukiona mauaji mengi ya Kigaidi yamekuwa yakitendwa na wenzetu wa kisilamu (Muslims) tukubali au tukatae Aibu na Ukweli upo pale pale!!!!!!!!!! Nadhani hata wewe unalijua jambo hilo?! Inasikitisha sana. Mungu tunakuomba ubariki Dunia yoote na ulete Amani na Upendo kwa Dini zoote.
Post a Comment