TAARIFA YA DUNIA KUHUSU MAKAZI YA BINADAMU 2013
Imewasilishwa na Bw. Phillemon Mutashubirwa
Mwakilishi
wa UN Habitat, Tanzania, Katika kuadhimisha siku ya makazi Duniani 7 Oktoba 2013
Kwa zaidi ya
nusu karne, nchi zina uzoefu wa ukuaji
wa haraka wa uchumi mijini na kuongezeka kwa matumizi ya vyombo vya
moto(k.m magari,pikipiki n.k). Hii imesababishwa na ukuaji holela wa miji na mahitaji makubwa kwa ajili ya usafiri
wa vyombo vya moto ambao una madhara mbalimbali
kimazingira, kijamii na kiuchumi.
Usafiri wa vyombo vya moto mijini ni chanzo kikubwa cha uzalishaji wa hewa ya ukaa ambayo inasababisha magonjwa kutokana na uchafuzi wa hewa, ajali zisizotarajiwa, msongamano na kelele n.k. Msongamano unaotokana na usafiri usio na mifumo endelevu ni wa gharama kubwa kiuchumi na hauna tija kwa wasafiri na bidhaa wanazosafirisha.
Usafiri wa vyombo vya moto mijini ni chanzo kikubwa cha uzalishaji wa hewa ya ukaa ambayo inasababisha magonjwa kutokana na uchafuzi wa hewa, ajali zisizotarajiwa, msongamano na kelele n.k. Msongamano unaotokana na usafiri usio na mifumo endelevu ni wa gharama kubwa kiuchumi na hauna tija kwa wasafiri na bidhaa wanazosafirisha.
Changamoto hizi, nyingi tunazikuta katika miji ya nchi zinazoendelea.
Toleo la mwaka huu la Ripoti ya UN-Habitat ya Makazi ya Binadamu duniani inatoa mwongozo juu ya kuendeleza mifumo endelevu ya usafiri mijini. Ripoti hii pia inaeleza mwenendo, hali ya mwelekeo na changamoto ya usafiri mijini na duniani kote.
Katika ripoti hiyo
umefanyika uchambuzi wa mahusiano kati
ya mfumo wa miji na uhamaji, na unatoa wito kwa ajili ya miji ya kisasa
inavyostahili kuwa hapo baadaye. Inaonyesha jukumu la mipango miji katika
kuendeleza miji endelevu ambapo usafiri wa umma usiokua wa vyombo vya moto
unapendelewa zaidi.
Ripoti inatoa mapendekezo namna gani taifa, mikoa na
serikali za mitaa na wadau wengine wanavyoweza kuweka mipango ya kuboresha na
kubuni usafiri endelevu mijini ili kupata nafuu sio kwa usafiri tu, bali pia
katika kutoa huduma, kuuza na kununua bidhaa zetu .
Makusudi mazima ya usafiri na uhamaji ni kufika
unapotaka kwenda, lakini iwe kwa bei nafuu na bila kuleta madhara. Ujenzi wa
barabara zaidi kwa ajili ya miji ya nchi zenye kipato cha chini ni muhimu sana
katika kutafuta suluhu la ufumbuzi wa usafiri endelevu, kwa hiyo ni muhimu sana
watu wa mipango miji kubuni miji itakayo
zingatia upatikanaji wa huduma zote sehemu moja, hivyo kupunguza umbali wa
kusafiri na kuongeza upatikanaji endelevu wa usafiri mijini. kwa mfano kama wakazi wa mijini wanaweza
kufikia upatikanaji wa huduma wanazohitaji bila kusafiri mbali au kupata huduma
hizo kupitia mitandao (mobile phone,online shopping) itasaidia kupunguza
changamoto za usafiri mijini. Ubunifu wa miji iliyo mchanganyiko kimatumizi
(mixed land use) italazimu halmashauri na serikali za mitaa zijenge miundombinu
rafiki na muafaka, zitunge sheria na kanuni za kuhakikisha watu wanaishi na
kufanya kazi karibu na maeneo yao.
Uwekezaji katika usafiri endelevu mijini ni muhimu
hasa katika nchi zetu zinazoendelea, ambapo idadi kubwa ya watu hawawezi kumudu
kulipa nauli inayohitajika kutumia usafiri wa umma, au kununua baiskeli.
Wengine wanaweza kumudu njia hii ya usafiri wa gharama nafuu, lakini si chaguo
lao kwa sababu mbalimbali, kwa mfano ukosefu wa miundombinu sahihi na usalama
wakati wa kuendesha baiskeli. Uwekezaji
katika miundombinu kwa ajili ya vyombo vya moto vilivyo nafuu ( na kukubalika),tukiwa
na mifumo mizuri ya barabara usafiri wa umma ni sahihi zaidi (na endelevu) na
mwisho wa siku hutumia fedha chache.
Hata hivyo nchi nyingi duniani zinapata matatizo
makubwa ya kitaasisi, kisheria na kiutawala zinapotaka kukabiliana na
changamoto za uhamaji mijini. Katika kushuhulikia changamoto hizi ripoti
inabainisha umuhimu wa kuhusisha wadau wote katika usafiri mijini (kama ngazi
zote za serikali, watoa usafiri na waendeshaji, sekta binafsi, asasi za kiraia
na watumiaji usafiri) kushiriki katika utawala na maendeleo ya mifumo ya
uhamaji mijini.
Ili kuleta ushirikiano wa usafirishaji na sera za
maendeleo ya miji ni muhimu kuoanisha usafiri mijini na sera za matumizi ya
ardhi [mixed landuse].
Mahitaji ya usafiri mijini ni makubwa kuliko kiwango
cha uwekezaji katika mifumo ya usafiri, Naamini ripoti hii itatumika kama mwongozo
kwa serikali za mitaa na wadau wengine
katika kukabiliana na changamoto za
mifumo ya usafiri mijini na duniani kote. Mwisho, ripoti hii inatoa ufahamu na
mawazo ya kuchochea ni jinsi gani tunaweza kujenga miji ya baadae itakayokua na
mifumo endelevu ya usafiri mijini, itaboresha kumfikisha mtu anapotaka kufika
na kutoa huduma nzuri kwa wakati mfupi inavyowezekana.
No comments:
Post a Comment