ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, November 12, 2013

Mkutano wa Tawi la CCM New York Metro (New York na Tri-State area PA, NJ & Ma)

Ndugu Wana CCM na Watanzania wote!

Yah: Mkutano wa Tawi la CCM New York Metro (New York na Tri-State area PA, NJ & Ma)

Tunapenda kuwakumbusha tena kwamba Tawi letu la CCM hapa lilifunguliwa rasmi Agosti 25, 2012 na Mh. Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM-Taifa.
Mkutano wa Wanachama wote ni Jumapili saa nane na nusu mchana (2:30 pm)Novemba 17, 2013.

Mahali: 2031 Adam Clayton Powell Blvd.(7th Ave. Between 121st and 122nd) Harlem, New York.

Tutakuwa na burudani ya muziki pamoja na karamu maalum kwa wahudhuriaji wote.
Tunaomba yeyote anaependa kujiunga na Chama au ni Mwanachama tayari wasiliana nakamati maalum.
1. Isaac Kibodya - Tel.(413)219-1153

2. Prof. Kamazima Lwiza - Tel.(631)278-3859

Kidumu Chama Cha Mapinduzi!

Uongozi wa Tawi  CCM New York!
Katibu wa tawi la CCM New York bwana Shaban Mseba akimkabidhi kadi ya CCM kada namba moja bwana Seif Akida.

Makabidhiano hayO yalifanyajika kwenye Ofisi ya tawi la CCM New York City
Mwenyekiti wa tawi la CCM New York bwana Mafutah alivyotembelea Ofisi ya tawi la CCM Lumumba Dar-Es-Salaam Tanzania.

Bwana Mafutah Mwenyekiti wa tawi la CCM New York akiwa na bwana Innocent Pila mwenyekiti wa tawi la CCM Lumumba wakipata ukodak. 

16 comments:

Anonymous said...

kumbe magamba wako pia new york nilidhani balaa hili lipo maryland na washington tuu kwa sabbau watanzania wa huko kwa kujirusha wananafasi na mambo kama haya sijajua new york wako nao magamba ebwaaa eeeh hii kali luke dj tupe tupe mambo muruwaaaaaa safi sana imekaa poa. magamba wa new york oyeee ha ha ha kazi ipo hata majuu magamba

Anonymous said...

Mkutano mkuu wa USA Democratic Party tawi la Tandika mikorosheni utafanyika jumapili saa 10 jioni. Wote mnakaribishwa.

Anonymous said...

Na sisi wa UK Labor Party tutafanya mkutano hapo Uvinza Reli stesheni leo jioni 30 Oktoba 2013.

Anicetus said...

Globalized world means
Freedom of free expression: respect- justice-beneficence

Anonymous said...

Nendeni mkachaharike nyie, mnaishi maisha ya Tanzania ugenini? Acheni uvivu

Anonymous said...

Fanyeni kazi nyie hizo kazi waachieni wenye nazo. Kazi kwa bidii na kuweka akiba sio msiba ukitokea kwenye akaunti zero afu tunaanza kuhangaika na michango namna ya kuufikisha msiba nyumbani. Na kama kazi hamna ludini nyumbani mkagombeee vizuri uongozi wa chama. Wabongo bwana porojo kibao mara buuu tunashindwa kwa kukimbilia bali msaada tutani. Mmmmmmh noumaaaa kweli kweli.

Anonymous said...

Alie kuambia hatuna kazi ninani usije ukaachwa nyuma usa wanaitangazia tanzania kwa maemdelo wewe mjinga unae filiria maisha ya ki tananzani hayana maana huo ni ulimbukeni wa ki jinga mshamba wewe tanzania juujuu na ccm juu zaidi

Anonymous said...

Kazi zilizo waleta kufanya zinawashinda mnatafuta kick za kuludi nyumbani si bora nika flip burgel mcD kuliko kwenda kwenye mikutano isio ma maana hacheni hizo

Anonymous said...

Ukisikia kukosa kazi ndio huku kwani nyumbani tz mmefukuzwa?

Anonymous said...

Mmmmmmh. Hatar kweli kweli.

Anonymous said...

Hamna lolote jamaa wote tunawajua hawana kazi zozte kushinda kwenye mikutano mara ya ccm mara
ya party ya mtu harusi kazi mnafanya saa ngapi ,bbq mpo hacheni hizo tushachoka peleka vyama huko tanzania kila nchi duniani wakifungua matawi ya vyama vyao tanzania mtawakubalia

Anonymous said...

AISEE EBU ACHENI USANII TAINGIA LINI WATU WANAGAWIANA KADI KIOLELA KAMA NYUGU KWENYE NYUMBA YA MTU,NA MANAYUZUGA KWA KUBANDIKA SKAFU YA CMM KWENYE UKUTA NA BAADA YA KUGAWIANA KTK OFISI YA TAWI LA CCM,JAMANI KAMA KUGANGA NJAA UNAWEZA UKAGANGA ATA NYUMBANI NA SIYO LAZIMA UGANGIE NEW YORK,MANAKE SIJUI ATA OFISI KAMA YA TAWI LA CCM NEW YORK IPO,ZAIDI YA JUGEUZA MIJENGO NA MAGETHO MNAYOISHI YA KULIPIA KUWA OFISI.JAMANI TUACHENI KU UNGA UNGA KUMBUKENI KILICHOWALETA MAREKANI
MASHAURI(MONTEGOMERY)

Anonymous said...

Well said, haya matawi ya CCM etc etc yana maana gani haswa? Rudini Bongo mkagombee uongozi 2015.

It makes me sick to see people wasting their time and resources on these CCM and Chadema crap!

Anonymous said...

mdau wa pili juu umeongea ukweli niko pamoja na wewe hivi nyie mmeshasikia USA Democratic Au republican wana matawi Bongo,Mfano kama Mdau alivyosema USA Democratic party Tandika Mikoroshini,Magomeni au manzese...haimaanishi kuwa bongo hamna wamarekani,Wapo sana ila hawakuona tija ya kufungua matawi hayo.kama wewe kweli unauchungu na TZ siurudi bongo ukafanye siasa,Uku New york Au DMV unampigia kampeni nani ya kugeuza nyumba mnazoishi na famila zenu kuwa Matawi ya CCM.Ebu Acheni Upuuzi huu
Asanteni.
Ronn

Anonymous said...

mimi naungana na Mashauri(Montegomery)msifanye vitu kisanii nyumbani kwa mtu kila kitu hapo hapo CCM ni chama cha wanachama sio cha mtu binafsi sasa huyo mwenye nyumba hata akigombea akishindwa siatafunga nyumba yake?pili unaposema mkutano wa CCM halafu unasema kila mtanzania aje sasa huo utakuwa wa CCM au watanzania?mkutano wa CCM maaana unazungumzia masuala ya CCM sasa mimi mtanzania halafu Chadema nikija nisikilize siri za CCM?...hebu acha usanii ndugu yangu wa Harlem

Anonymous said...

asiye take kujaa hamlazimishwi kila mtu anaakili zake za kuzaliwa ukona ku flip burger mcdonald ndo deal fanya hivyo ukiona kuja katika mkutano ndo deal fanya hivyo unauhuru wa kufanya unachotaka hulazimishi acheni zenu za michongo kila mtu amekuja huku majuu kwa akili zake mwenyewe na uwezo wa mungu so msijifanye mnajua sana maisha ya kutafuta pesa na kuona mambo haya ya kijinga hamlazimishwi hakuna anayekuhitajini kwa sana ndo maana mnakufa kwa stress hajui kufurahi wala kuburudika kila siku mikazi mikazi mpaka mnapata maugonjwa bila sababu furstration hizo.
kila la kheir na ku flip burgers na kupiga maboksi na kuchuma kwa pesa kila kona msichoke tu kuna siku mtahitaji kuja home na vyama ndo hivyo tena karibuni lakini hamlazimishwi.