Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa jengo la halmashauri ya mji wa Kibaha jana. Kushoto ni Mbunge wa Kibaha mjini Mhe. Sylvestry Koka.
Mwakilishi wa Serikali ya Cuba ambaye pia ni Mkuu wa Shirika la Utafiti la LABIOFAM Dk. Jose Antonio Fraga Castro (kushoto) pamoja na Balozi wa Cuba nchini Tanzania Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo wakimkabidhi Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere akiwa na Rais kiongozi wa Taifa la Cuba Fidel Castro wakati wa uwekaji jiwe la msingi kiwanda cha Viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza Malaria katika hafla iliyofanyika Kibaha mkoani Pwani jana.Wa pili kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdallah Kigoda. Mradi huo utaendeshwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya watu wa Cuba.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mbunge wa Kibaha mjini Mhe. Sylvestry Koka wakikagua jengo la halmashauri ya mji wa Kibaha muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuweka jiwe la msingi huko mjini Kibaha jana. Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi mkoani Pwani.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wananchi waliofurika katika Viwanja vya CCM, Mlandizi ambapo aliwahutubia katika mkutano wa hadhara.
Rais Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi katika Viwanja vya CCM, huko Mlandizi, Kibaha mkoani Pwani.
(PCHA NA FREDDY MARO)
No comments:
Post a Comment