Familia ya Yagaza ya Korogwe, Tanga inasikitika kutangaza kifo cha mtoto wao mpendwa Mwl. Osckar Yagaza uliotokea siku ya Jumatatu, Oktoba 28, 2013. Shughuli za mazishi zitafanyika siku ya Alhamisi Novemba 7, 2013 nyumbani kwao Manundu Korogwe.
Wana-Yagaza USA watakuwa na mjumuiko wa sala ya Misa Takatifu kumuombea marehemu siku ya Ijumaa Novemba 1, 2013 saa 11 jioni nyumbani kwao 16 Robinson Street Binghamton, NY.
Raha ya milele umpe ee Bwana na mwanga wa milele umuangazie apumzike kwa amani, amina."
No comments:
Post a Comment