NCHI za Tanzania na Burundi, kwa mara nyingine zimetengwa na wenzao wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), baada ya marais wa Kenya, Uganda na Rwanda kukutana mjini Kigali jana. Marais hao walitarajia kujadili namna ya kuimarisha Jumuiya ya Afrika Mashariki kupitia uimarishwaji wa miundombinu, uchumi, biashara pamoja na kuweka mikakati ya shirikisho la kisiasa.
Kitendo cha kuziacha Tanzania na Burundi ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kinazidi kutia shaka mtangamano wa jumuiya hiyo.
Nchi hizo mbili zimeshaeleza kusikitishwa na muungano wa nchi hizo tatu, ambao zimesema unakwenda kinyume cha makubaliano na mkataba wa EAC.
Katika mkutano huo, marais hao, Paul Kagame wa Rwanda, Yoweri Museveni wa Uganda na Uhuru Kenyatta wa Kenya, pamoja na mambo mengine, walitarajia kusaini makubaliano ya kuanzisha kituo kimoja cha kukusanya ushuru kinachotarajia kurahisisha uchukuzi wa bidhaa kutoka Mombasa nchini Kenya, Uganda hadi Rwanda.
Aidha Sudan Kusini ilialikwa ikiidhinishwa kama mshirika katika kikao hicho.
Mkutano huo unakuja baada ya ule uliofanyika mjini Kampala, Uganda, Juni mwaka huu na mwingine uliofanyika Mombasa, Agosti, ambako viongozi hao watatu walipendekeza kupanuliwa kwa Bandari ya Mombasa, ili kuwezesha uharaka wa bidhaa kupitishwa katika kuhudumia kanda nzima.
Mkutano mwingine wa marais wa nchi 15 za Afrika, ikiwamo Tanzania, utafanyika leo nchini hapa, katika kongamano la siku nne ambalo linatarajiwa kuweka kipaumbele kwa uimarishwaji wa huduma za internet katika mataifa hayo.
Kwa mujibu ya waandaaji, zaidi ya wajumbe 1,500 watahudhuria mkutano huo, chini ya uenyeji wa Rais Paul Kagame na Dk. Hamadoun I. Toure, Katibu Mkuu wa Muungano wa Kimataifa wa Mawasiliano ya Kiteknolojia (ITU).
-Mtanzania
10 comments:
Hao wote ni wanafiki. Sioni kwa nini Tanzania isijitoe na huu umoja wa EAC? Jomo Kenyatta aliuuwa Umoja huo miaka ya sabini. Na leo mwanae Uhuru analiongoza kundi la wanafiki ambao hawaipendi Tanzania. Nadhani serikali yetu imelitambua lengo la hao wanafiki. Tupo imara Tanzania, na tutasonga mbele bila wao, wamesahau kwamba tumewakomboa katika vita na tunawalisha vyakula vyetu. Watanzania ni shupavu, na Mungu ibariki Tanzania.
sisi watanzania hatuhitaji huo muungano ili tuweze kuendelea mi naona bora tujitoe tu SADC inatutosha. wacha tuone watafikia wapi.
Hata nami nakuunga mkono. kuna mambo hayafai kufumbiwa macho hata kidogo. Kama swala linahusu EAC, iweje wasishirikishwe kwenye hivyo Vikao?? na badala yake kuitana kinyemele....ukweli utajulikana tu nini nia yao.
acha kujidanganya wewe, the question is why its happen? ukiona watu wanafanya hivi ujue kwamba wameona uko weak. Watu na Viongozi wa tanzania are weak,especially president is very weak and not smart. we need to open up our eyes and be honest to ourselves. learn from our mistake
They can do it without us, we can do it without them. So let it be written, let it be done.
Musevini ni dikteta,Kagame ni muuaji,Uhuru ni jambazi/muuaji.Kwa TZ kundelea ndani ya EAC Ni sawa na Njiwa ndani ya muungano wa Mwewe,Kipanga,na Kunguru.
HAYA MAJAMAA HAYANA SHUKRANI ISINGEKUWA UONGOZI BORA NA SERIKALI IMARA YA TANZANIA LEO WASINGEKUWEPO MADARAKANI KUANZIA UGANDA TULIWATOLEA IDD AMINI NDULI MLA WATU NA KUWASAIDIA KUJITAWALA KIDEMOKRASIA, SAME WITH KENYA TULIWAPOKEA WAKIMBIZI KIBAO WAKATI WALIPOKUWA WANAUANA KAMA KUKU AND SAME WE DID FOR RWANDA AND BURUNDI, NYERERE NA VIONGOZI WOTE WA TANZANIA YOU SHOULD FEEL PROUD OF THE CONTRIBUTION AND SACRIFICE WE MADE FOR THESE PEOPLE AMBAO SASA WANAJIDAI ETI KUTUTENGA. LETS WATCH HOW LONG THEY WILL SURVIVE!!! TUNAJIVUNIA NCHI YETU JAMANI HII WALA HAININYIMI USINGIZI ITS A MATTER OF TIME UTASIKIA WAMETIMUANA YOU ALL JUST WATCH.
Kagame na Uhuru wote wanatakiwa the Hague.. Tusijifanye wakarimu Sana kuwatetea!! Mnaona matokeo ya kujifanya uAfrica mbele? Tucheze kivyetu Tanzania mbele!! Muungano wetu unatusumbua tunatafuta muungano na Manyang'au !!
WW annon unaesema watanzania na rais wetu tuko weak ni ww na familia yako ndo mko weak usiingize watu wote..hao wakenya,warwanda na waganda wanatuzidi kwa lipi hasa???acha waendelee na muungano wao wa mashaka na sisi tutajikita zaidi na SADC..tuone nani atapoteza ...tunaomba serikali yetu itoe tamko rasmi la kujitoa na hii EAC..Tanzania kwanza!
u can't handle the truth, that the sign of weakness, take it or leave it, Don't take it personal, we are very weak and not smart. open your eyes
Dhambi ya Ubaguzi ni Mbaya Kuliko dhambi zote,,Tuwangalie hawa watu watatu,,Kinyata na Kagame wanadhambi kubwa ya mauaji ya kikabila,,Mseven jeshi lake limekuwa likibaka wanawake na watoto Congo,,sasa watu wenye mawazo hovyoo namna hii ,,hawatufai kabisa
Post a Comment