ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, October 5, 2013

WILLIAM MALECELA "NITAIRUDISHA KADI YANGU YA CCM SIKU WABUNGE WAKIRUDI BUNGENI NA KUBADILI MAAMUZI JUU YA KATIBA"


Katika hotuba ya Rais jana amesema Wabunge warudi tena Bungeni kujadili tena Muswaada waliokwisha upitisha tayari kwa mujibu wa sheria ya Jamhuri ya Muungano ya Taifa Tanzania, well sina tatizo na Wabunge kurudi Bungeni kujadili tena lakini iwapo Wabunge wa CCM watabadili msimamo na kukubali ambacho hawakukitaka mwanzoni, NINAKIAHIDI CHAMA CHANGU CCM KWAMBA NITAKUWA WA KWANZA KURUDISHA KADI YANGU, RASMI.
- Kuna wakati siasa zinatakiwa kufika to a dead end, na here we are, nasema tena sina tatizo na Wabunge kuombwa kurudi Bungeni na Rais wa Jamhuri, lakini nitakuwa na tatizo kubwa iwapo Wabunge wangu wa CCM watabadilika na kuweka msimamo mpya badala ya ule walioupitisha tayari kwa mujibu wa sheria, naahidi kwa Miungu yangu yote kuwa NITAIRUDISHA KADI YANGU YA CCM SIKU HIYO HIYO FASTA SANA!!

- CCM NI CHAMA CHA MAPINDUZI I MEAN REVOLUTION SIO ANYTHING ELSE, NAWAKUMBUSHA WABUNGE WETU WA CCM KWAMBA WANACHAMA WAKE TUNATAKIWA WANA MAPINDUZI NA WENYE MSIMAMO SIO WAOGA WAOGA WAKUYUMBISHWA YUMBISHWA NA THIS IS BEST TEST EVER!!!

- KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!! CCM!

Le Mutuz

14 comments:

Anonymous said...

Ndiyo maana hauko bungeni... Kijana kama wewe ni hatari kwa nchi yetu: ( Uongozi ni busara na busara haiko kichwani mwako... Tunaandika katiba kwa hiyo kila penye kutoeleweka panahitaji masahihisho ..JK si mjinga kama wewe ana busara ndiyo maana hakusaini !! Usicheze na katiba... Katiba mbovu ni mwanzo wa siasa chafu ....

Anonymous said...

unamtisha nani bwana mdogo rudisha tu hiyo kadi yako kwani wewe ndo nani hasa halafu si unatafuta umarufu kuuza sura. rudisha nenda kajiunge na vyama vya upinzani unadhani hatujui ajenda yako,pombe za mnazi zinakutia wazimu siku hizi rudi u.s.a ulipotoka

Anonymous said...

ah! achen misimamo ya banyamulenge! wabunge kurudi bungeni ni ushauri wa Mh. Rais wetu for the interest of the majority! so far katiba sio kwa ajili ya CCM! ni kwa ajili ya majority ya watanzania, hata hvo kwa mtu ambaye amelelewa ktk mazingira ya kupanda ndege hata kama anapelekwa shule ya awali, kutibiwa mafua India na Ulaya cdhan kama atakua na uchungu na matokeo ya katiba mbovu!!! C'com! LET US AGREE TO DISAGREE!

Anonymous said...

Nawewe nenda kajipikilishe uko,kuwa mwanachama au kujitoa ayatuhusu

Anonymous said...

Rudisha kadi yako, wewe ni mmoja kati ya watanzania mil 46. CCM mna tabia ya kulewa madaraka, mnaona kabisa haki haikutendeka, Rais mwenyewe ameona kuna shida wewe unakataa. Unajua na umeona zanzibar haikuhusishwa lakini unavutia upande wako. Sisi tunaongelea demokrasia wewe unaongelea mapinduzi, mapinduzi gani hayo unayoyasema? Ni bahati mbaya sana Africa imejaa watu kama wewe ndiyo maana tumebaki wa mwisho kwa sababu watu kama wewe wanajijali wao peke yao.

Anonymous said...

Napenda kukupa ongera willy malecela .Bunge haliwezi kuchezewa. Na msimamo wako ndio msimamo unao takiwa na viongozi au kiongozi ili uwe kiongozi ndio unatakiwa kuwa na msimamo . kiufupi umenifurahisha sana na umenipa nguvu kwamba angalao tuna viongozi wenye msimamo katika Tiafa letu.

Anonymous said...

It’s very sad to have a very narrow opinion coming from someone who said that he has a Political Science Diploma from Community Collage and then he can not distinguish the meaning of "Revolution".

We did not get our independent through the barrow of the gun!! that did not happen pure and simple.

So for you to think that you’re a revolutionary because you belong to CCM it is very sad, very sad indeed. Return your card and no one will care late alone notice the incident.
In politics there are give and take to reach compromise and let me remind you that this new Constitution it is NOT a CCM agenda, it is a Citizenry issue it`s belong to every single Tanzanian who really care about t Country.

You have very narrow opinion just like your father, that’s why your father was pushed out of the ruling Clad, even your our people could not bring themselves to vote for him !! It`s sad that you haven`t learned from your fathers mistakes.
And I guaranteed you that, they are going to change they are opinion for the sake of the country not for the sake of the CCM, no body really care about what you thing or say.

FYI:

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Those words are just a party slogan nothing much.

Anonymous said...

nataka kujua jamaa huyu kama nani ccm please wadau nielezeni

Anonymous said...

Siku zote nilikia nadhani ni Zanzibar tu ndiko kuliko na maborafya siasa chuki kumbe na Tanganyika munao!!!!?. Duh poleni.

Unknown said...

Kwa mazungumzo ya huyu jamaa haraka haraka, nimemsoma personality yake, ni type ya wale watoto wa wakubwa waliopelekwa kusoma kwa kodi za wananchi, lakini haina maana up stair iko vizuri. Uwezo wake wa kufikiri ni mdogo sana. Nina wasiwasi hata hako kadigrii kama aliperfom vizuri, maana uwezo wake wa analysis wa yale anayoongea hauendani hata na kuchambua hadhira yake ina upeo gani (Audience. Unajua hajui hata audience yake ina upeo gani. Siku hizi maelfu ya watanzania wanakwenda kusoma vitu vya maana huko nje na wana upeo mkubwa. Ninachokiona kwa haraka ni kwamba William anaweza kuwa mratibu mzuri wa mashindano ya Urembo, Kuratibu ratiba za bendi za muziki lakini si kuwa kiongozi. Hivi hawa watu mnawatoa wapi,Hebu angalia watu walioelimika kama JANUARY MAKAMBA. unapata impression huyu kaelimika.

Anonymous said...

tena rudisha hata kesho kwani wewe ndio nani?ukirudisha kwani watu watapungukiwa na nini?shukuru sana hiyo last name uliokuwanayo.

Anonymous said...

rudisha hata kesho kwani wewe ni njia watu watashindwa kupita?shukuru mungu hiyo last name yako ndio inakuweka mjini.

Anonymous said...

rudisha hata kesho kwani wewe ni njia watu watashindwa kupita?shukuru mungu hiyo last name yako ndio inakuweka mjini

Anonymous said...

huyu bwana ni aibu kuitwa mtoto wa Mh Samwel Malecela, mbona idealogy hazifanani na msomi wala muelewa!!