ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, November 30, 2013

KINANA AWA SHUJAA CHUNYA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia ujenzi wa barabara ya Mbeya-Chunya unavyoendelea,kulia kwake ni Meneja wa Tanroads mkoa wa Mbeya Mhandisi James Nyabakari,na Mhandisi wa kampuni ya China Communication Construction Construction kutoka China Mr.Jobs Lin ,wengine pichani ni Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro ,Mwenyekit wa CCM Mkoa wa Mbeya na Mbunge wa Mbozi Ndugu Godfrey Zambi na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
Ujenzi wa Barabara ya km 36 ukiendelea barabara hiyo inaunganisha Mbeya na wilaya ya Chunya na baada ya hapo itaunganisha mpaka mkoa wa Tabora .
Kijana Frank Robert Mwapololo ambaye anafanya shughuli za uchimbaji madini katika kundi la wachimbaji wadogo akirejesha kadi ya upinzani kwa Katibu Mkuu baada ya Katibu Mkuu kutembelea kituo cha mafunzo cha wachimbaji wadogo cha Matundasi na kufanya mazungumzo na wachimbaji hao ambao walitoa malalamiko yao juu ya gharama za leseni,riba ya mkopo na utaratibu mzima wa kupata mkopo ni mgumu kwa hasa kwa mtu anayeishi vijijini pamoja na ukosefu wa vifaa vya kuchimbia.

Aliyekuwa Katibu wa Chadema Wilaya ya Chunya Brayson Mwasimba akirudisha kadi yake na kujiunga rasmi na CCM baada ya Katibu Mkuu wa CCM kuhutubia kwenye viwanja vya Lupa, wilaya ya Chunya.


Brayson Mwasimba akionyesha kadi yake mpya inayomuonyesha yeye ni mwanachama wa chama cha Mapinduzi sasa, Brayson alikuwa Katibu wa Chadema wilaya ya Chunya amekiri alipotea kujiunga Chadema na akaomba wanachunya wamsamehe mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Lupa wilaya ya Chunya.

MAMBO YANAVYOENDELEA SASA HIZI MISS TANZANIA USA PAGEANT

Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula akiwa meza kuu na Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn. Iddi Sandaly kwenye ukumbi wa Hollywood Ballroom kunafanyika Miss Tanzania USA Pageant sasa hizi ukumbi upo Silver Spring, Maryland.
 Balozi Mulamula akisalimiana na majaji wa Miss Tanzania USA Pageant mara tu alipowasili ukumbini hapo.
 Mhe. Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Miss Ambassador
 Mhe. Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Miss Sierra Leone
 Mhe. Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Jaji Peter Walden
 Mhe. Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na aliyekua Miss District Of Columbia
Mhe. Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Miss America
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Bwn. na Bi Matope.
Mlimbwende Jessica kutoka New York akiwakilisha ndani ya nyumba.
Mlimbwende Koku naye yupo ndani ya mjengo.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi

Kapteni Mstaafu Robert: Sitasahau nilipohukumiwa maisha jela

Rubani wa ndege aliyeonja kifo kwa ajali ya ndege na kifungo cha maisha, Rubani huyu ni Kapteni Mstaafu Rodrick Robert (69). Picha na Maktaba

Nje kidogo ya Mji wa Songea, kipo kijiji kinachoitwa Mateka. Bila shaka jina la kijiji hicho lina historia yake, lakini kubwa ni kwamba ndiko anakoishi rubani wa ndege aliyeonja kifo kwa ajali ya ndege na kifungo cha maisha.
Rubani huyu ni Kapteni Mstaafu Rodrick Robert (69) mrefu, mweupe ambaye si mnene na wala si mwembamba akiwa na nywele laini zinazoashiria wazi kwamba mmoja wa wazazi wake alikuwa mtu wa nje ya Bara la Afrika.

KUTIMULIWA ZITTO, Dk. Kitila CHASO: Uamuzi wa CC Chadema ni muafaka

Lawarushia shutuma waliofukuzwa BAVICHA
Suala la kutimuliwa kwenye madaraka ya uongozi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Zitto Kabwe, na Mwanazuoni kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitila Mkumbo, sasa limechukua sura mpya.

Shirikisho la wanachama wanafunzi wa Chadema kutoka vyuo vya Elimu ya Juu, mkoa wa Dar es Salaam (Chaso), jana limeibuka na kuunga mkono uamuzi wa Kamati Kuu Chadema kuwavua uongozi waliodaiwa kufanya uasi ndani ya chama

Shirikisho hilo pia limewarushia shutuma Mtela Mwampamba, Habib Mchange, Juliana Shonza na Greyson Nyakarungu, waliofukuzwa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha), kutengeneza makundi ya kupinga uamuzi uliofikiwa na Kamati Kuu hiyo.

GEORGE ZIMMERMAN STILL HOUNTED BY TRAYVON KILLING



                   MOHAMEDMATOPE
Last August, I wrote a column expressing my disappointment in George Zimmerman’s trial after he was acquitted of the criminal charges that resulted from his 2012 killing of Trayvon Martin.

 I wrote that column with the intent to spark debate specifically to the American audience on at a time already heated nationwide debate about race and self-defense and overall justice system.  But, I didn’t know if the story of a murdered black teenage in Florida would strike a chord with a wider audience. I received hundreds of emails and comments from many peoples around the world; many of whom were puzzled, particularly with the American’s gun laws.

Ndege iliyopotea Msumbiji yapatikana

Ndege hiyo ilitakiwa kutua kwenye uwanja wa Luanda.

Ndege iliyopotea tangu jana baada ya kuruka kwenye anga ya Msumbuji kuelekea Angola ikiwa na watu 34 imepatikana katika mbuga za wanyama Kaskazini Magharibi mwa Namibia.

Msemaji wa Polisi nchini Namibia amesema ndege hiyo iliteketea yote huku kukiwa hakuna aliyenusurika.
Ndege hiyo namba TM470 iliondoka Maputo nchini msumbiji tangu siku ya ijumaa na ilikuwa ikielekea Luanda nchini Angola.

Temptation, Diamond Platnumz & HHP, Coke Studio Africa

TAZAMA PICHA DIAMOND AKITUMBUIZA KWENYE UJIO WA KOMBE LA DUNIA TANZANIA@HOTEL SERENA

 viwanja vya hotel ya
Serena jijini Dar ,na
mimi kama barozi wa Coca cola nilikuwepo na nilipangwa
kama mmoja ya wasanii wa Kitanzania tuliotumbuiza
Home sweet home,nikijiandaa.........
My personal security officer,call him Mwarabu akiwa satandby kabisa akinisubili...
Baada ya kuwasili hotelini@Serena hotel,kulikwa
na ulinzi wa hali ya juu sanaa.........
Tukikwea ngazi kuelekea kwenye vyumba vyetu

MSAFARA WA MWENYEKITI UVCCM WAWEKEWA MAGOGO

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) taifa, Sadifa Juma Khamis (MB) Polisi mkoani Pwani inachunguza kundi la watu linalodaiwa kuweka magogo barabarani kuzuia msafara wa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) taifa, Sadifa Juma Khamis (MB) katika eneo la Tondoroni, wilayani Kisarawe, mkoani humo. 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Ulrich Matei, alisema atazungumzia suala hilo baada ya kupata taarifa kamili.

IGP SAIDI MWEMA ATANGAZA MABADILIKO KATIKA JESHI LA POLISI TANZANIA

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema amefanya mabadiliko ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera pamoja na baadhi ya Wakuu wa Upelelezi wa mikoa na wakuu wa Polisi wa Wilaya katika baadhi ya mikoa hapa Nchini. 
Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Philipo Kalangi amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam, kuwa Mkuu wa kikosi cha kusimamia usalama wa Mazingira na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) George Mayunga ambaye alikuwa Mkuu wa kikosi cha kusimamia mazingira Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam. 
Aidha, baadhi ya Wakuu wa Upelelezi wa mikoa (RCO) na wakuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) waliobadilishwa ni pamoja na 
aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Tabora ACP Edward Bukombe amehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam, Mkuu wa Upelelezi wa mkoa wa Geita (RCO) ACP Francis Kibona amehamishiwa mkoa wa Njombe kuwa mkuu wa Upelelezi mkoa na nafasi yake inachukuliwa na SSP Simon Pasua kutoka Makao makuu ya Upelelezi Dar es Salaam. 
Wengine ni aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) ya Wanging’ombe SSP. Francis Maro amehamishiwa Mkoa wa Katavi kuwa Mkuu wa upelelezi wa mkoa na aliyekuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Katavi ACP. Emmanuel Nley amehamishiwa kikosi cha Polisi wanamaji Dar es Salaam. Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Rukwa SSP. Peter Ngussa amehamishiwa Makao makuu ya Upelelezi Dar es Salaam, nafasi yake inachukuliwa na SSP Alan Bukumbi aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Njombe. 
Aliyekuwa Mkuu wa Polisi wilaya ya kati( OCD) Mrakibu wa Polisi (SP) Salum Ndalama anaenda kuwa kaimu mkuu wa upelelezi mkoa wa Tabora na aliyekuwa mkuu wa Polisi wa wilaya ya Tunduru (OCD) SP. Amadeus Tesha anakwenda kuwa Mkuu wa upelelezi kikosi cha Polisi reli. 
Uhamisho huo ni wa kawaida katika kuboresha utendaji kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi. 
Imetolewa na: Advera Senso-SSP Msemaji wa Jeshi la Polisi.

JK AMUWEKA KITANZINI PROFESA KAPUYA

RAIS Jakaya Kikwete ameviagiza vyombo vya dola kuhakikisha vinamkamata mtu yeyote bila kujali cheo, atakayebainika kumbaka au kumuoa mwanafunzi wa shule.

DIAMOND PLATINUMZ APIGWA MADONGO VIBAYA NA BABY MADAHA!

MSANII filamu na muziki wa kizazi kipya wa Tanzania Baby Joseph Madaha maarufu kwa jina la (Baby Madaha) amesema kwamba msanii mwenzake wa muziki nchini,Naseeb Abdul maarufu kwa jina la Diamond Platinumz si msanii bali ni mfanyabiashara.

SABABU ZA KWANINI WABUNIFU WENGI WA KIUME WA MITINDO NI MASHOGA

Tom Ford
Pointi ya msingi: Upenzi wa mashoga katika urembo, utanashati hauwezi kuelezeka. Inasemekana kuwa mwanaume anayebuni nguo nzuri kwa mwanamke aidha hutaka kuwa na mwanamke ama hutaka kuwa mwanamke’
Bila shaka umeshajiuliza sana kwanini wabunifu wengi wa nguo wa kiume duniani ni mashoga. Haya ndio majibu:
Kwanza, tasnia ya mitindo (fashion industry) kiutamaduni imekuwa ikiwakubali zaidi mashoga wanaojulikana wazi (openly gay men) tofauti na fani zingine. Hata leo, ni changamoto kubwa kwa shoga kufikia level ya kuwa CEO ama Mkurugenzi kuliko wanaume wa kawaida.
Tofauti ni kwamba shoga kwenye fashion anaweza kuheshimika na kuenziwa kwenye fani hiyo na kufanikiwa binafsi na kifedha bila kudhihakiwa kama ambavyo anaweza kujikuta akifanyiwa kwenye fani zingine kama upolisi, jeshi na kwenye michezo.

MSANII TID ATUPWA MAHABUSU KWA KOSA LA KUMPIGA DEMU WAKE

Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Khaleed Mohamed 'TID' yupo mahabusu katika Kituo cha Polisi Oysterbay tangu jana usiku baada ya kukamatwa na polisi kwa tuhuma za kumpiga na kumjeruhi msichana anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake, Mariam Nnauye.

VIJIMAMBO WATOTO-gnomeo and juliet full movie

ALI KIBA "NI WAKATI WANGU WA KUAMKA KATIKA USINGIZII ULIYOJAA MAUMIVU NA DRAMA"


Hitmaker wa Cinderela na Dushelele, Ali Kiba ambaye leo anasherehekea birthday yake ya kutimiza umri wa miaka 27, amefunguka kwa kusema alikuwa kimya kutokana maisha ya muziki anayosema yamejaa drama, mateso na mambo mengi.
 Ali Kiba amesema muziki wa Tanzania umejaa drama zilizomfanya atulie kidogo kutafakari na ili kusudi ajue jinsi ya kukabiliana na changamoto zake.

CHEGE, TEMBA NA BI CHEKA WAWA VIVUTIO VIKUBWA LEO KATIKA UWANJA WA TAIFA WAKATI WA ZIARA YA KOMBE LA DUNIA

Mh Temba na Chege wakikamua vilivyo katika Steji ya Coca Cola Fifa trouphy tour iliyotua jijini Dar jana usiku na leo kuwa katika uwanja wa Taifa kwaajilii ya wakazi wa Jiji la Dar na Vitongoji vyake kuweza kupata fursa ya kupiga nalo picha.
 Chege, Temba na Wanaume TMK wakirusha mapanga shaa shaaa katika shoo ya Kombe la Dunia katika Uwanja wa Taifa leo
kwa picha zaidi bofya soma zaidi

Ushahidi wa umiliki wa Ziwa Nyasa watolewa

Watu wa viunga vinavyolizunguka Ziwa Nyasa /Ziwa Malawi wakiendelea na shughuli za uvuvi. Tafiti mbalimbali zimeonyesha wengi wao hawaelewi hasa chanzo cha mtafaruku huu wa mipaka ya Ziwa ulioibuka kati ya Tanzania na Malawi. PICHA | PLATOURS (KWA HISANI)

Dar es Salaam. Malawi na Tanzania zimewasilisha ushahidi na majibu ya maswali kuhusu umiliki wa maeneo kwenye Ziwa Nyasa, kwa jopo la wasuluhishi linaloongozwa na Rais mstaafu wa Msumbiji Joachim Chissano.
Wasuluhishi hao walizitaka Malawi na Tanzania kutoa majibu ya maswali manne muhimu, wakati wakiwasilisha ushahidi wao kuhusu umiliki wa ziwa hilo wenye mgogoro.

MAMIA YA WAKAZI WA JIJI LA DAR NA VITONGOJI VYAKE WAJITOKEZA KWA WINGI KWAAJILI YA KUPIGA PICHA NA KOMBE LA DUNIA MUDA HUU KATIKA UWANJA WA TAIFA


Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar na Vitongoji Vyake wakiwa katika mstari kwaajili ya kuelekea sehemu ya Kupiga picha na Kombe la Dunia katika Uwanja wa Taifa uliopo Wilayani Temeke Jijini Dar leo
Wakazi wa jiji La Dar wakiwa kwenye mstari tayari kwenda kupiga picha na kombe la Dunia lililopo jijini Dar leo katika uwanja wa taifa

Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake wakiwa ndani ya eneo la kupiga picha na kombe la dunia
Baadhi ya Raia wa Nchi za Nje wakiwa katika eneo la Kupiga picha na kombe la Taifa katika uwanja wa Taifa Muda huu

Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar wakiwa katika foleni kwaajili ya kusubiri Picha zao ambazo wamepiga na kombe la Dunia muda huu katika uwanja wa Taifa
kwa picha zaidi bofya soma zaidi

‘Viongozi utendaji dhaifu, kipato kikubwa’

Rais Jakaya Kikwete alinukuliwa katika kikao cha OGP London akisema mishahara ya viongozi wa umma haiwezi kuwa siri kwani ni sehemu ya bajeti, ingawa leo hii wengi katika serikali yake wanatetea usiri uliokithiri katika suala zima la vipato vya ‘wakubwa.’ PICHA | MAKTABA
Dar es Salaam. Ripoti mpya ya utafiti imebainisha kuwa mishahara mikubwa wanayolipwa viongozi wa juu serikalini na wanasiasa hailingani na utendaji wao wa kazi.
Ripoti hiyo iliyozinduliwa jana jijini Dar es Salaam, imeeleza kuwa viongozi hao wanalipwa mishahara inayotofautiana kwa kiwango kikubwa na pato la mwananchi wa kawaida.

MISS TANZANIA USA PAGEANT

Piga namba zifuatazo kupata ticket.