ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, November 28, 2013

BALOZI WA MAREKANI KATIKA UMOJA WA MATAIFA AMTEMBELEA BALOZI WA TANZANIA KATIKA UMOJA WA MATAIFA

Muwakilishi wa Kudumu wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Balozi Samantha Power jana jumatano ( Nov27) alifika katika Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, na Kufanya mazungumzo na mwenyeji wake, Muwakilishi wa Kudumu, Balozi Tuvako Manongi. Balozi Power alitumia fursa hiyo kujitambulisha kwa Balozi mwenzake kufuatia kuteuliwa wake hivi karibuni na Rais Barack Obama kuwa muwakilishi wake katika Umoja wa Mataifa. Katika mazungumzo yao yaliyochukua takribani nusu saa, Mabalozi hao wawili, walijadiliana na kubadilisha mawazo kuhusu masuala mbalimbali ya kimataifa na kitaifa yakiwamo ya uhusiano na ushirikiano wa karibu kati ya Tanzania na Marekani na vilevile walijadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu vipaumbele vya nchi zao katika Umoja wa Mataifa na namna ya kukuza na kuendeleza uhusiano na ushirikiano huo.
Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, akimkaribisha mgeni wake, Balozi Samantha Power ambaye ni Muwakilishi wa Kudumu wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Balozi Power alifika katika ofisi za Uwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumza na mwenyeji wake
Balozi Manongi na Balozi Power wakiangua vicheko, hapa ilikuwa ni baada ya Balozi Power kumtania Balozi Manongi kwa kusema " na wewe ulikuwa kati ya wale walioshangilia sana kwenye Baraza Kuu la Usalama?
Mazungumzo yakiendelea

No comments: