Dar es Salaam. Aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba ameeleza jinsi anavyojisikia furaha kustaafu, kwa kuwa atapata nafasi nzuri ya kuwa karibu na familia yake.
Akizungumza na Mwananchi kwa simu jana, Manumba ambaye amelitumikia Jeshi la Polisi tangu miaka ya 1970, alisema makazi yake yataendelea kuwa jijini Dar es Salaam
“ Nafurahi kwa kuwa nitapata muda sasa hata wa kucheza na watoto, bado sijajua mengine nitakayoyafanya ikifika siku nitawaeleza’ alisema’ DCI Manumba amelitumikia jeshi hilo katika nyadhifa mbalimbali zikiwamo katika Chumba cha Kupokea Mashtaka kati ya mwaka 1976 hadi 1977 na baadaye Mwendesha Mashtaka Wilaya ya Kibondo na Kasulu mkoani Kigoma kati ya 1977 na 1984.Manumba pia amewahi kuwa Mkufunzi katika Chuo cha Polisi kilichopo Kurasini Dar es Salaam, kati ya mwaka 1984 na 1987 kabla ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kipolisi ya Magomeni na Kinondoni. Manumba baadaye aliteuliwa kuwa Naibu Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuanzia 1987 hadi 1993.Kati ya mwaka 1993 na 1995, alikuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Arusha kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa wa Mkufunzi Mkuu wa Chuo cha Polisi Moshi kati ya 1995 na 1996.
Aliteuliwa kuwa Mkuu wa Kitengo cha Kukabiliana na Uhalifu wa Kughushi Makao Makuu ya Upelelezi mwaka 1996 na 1997 na baadaye kuwa Mkuu wa Kitengo cha Usalama, Intelijensia na Kupambana na Biashara ya Dawa za Kulevya kwenye Makao Makuu ya Upelelezi kuanzia 1997- 2001. Mwaka 2001- 2006 aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai na kuanzia mwaka 2006 hadi anastaafu, alikuwa Mkurugenzi wa idara hiyo.
Mwananchi

No comments:
Post a Comment