ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, November 14, 2013

DIAMOND KWENDA JELA,KISA MAMA YAKE JITIRIRISHE HILI UJUE KULIKONI

STAA wa Bongo Fleva,Naseeb Abdul’Diamond amefunguka kuwa yuko tayari kwenda jela kama atatokea mtu yoyote akamchezea au kumdhalilisha kwa namna yoyote mama yake mzazi Bi.Sanura Kassim.
Akizungumza kupitia kipindi cha Take One cha Clauds TV na Zamaradi Mketema hivi karibuni alisema kuwa ni bora hao watu wakamchezea yeye(Diamond) hasa waandishi wanavyomdhalilisha kwenye magazeti kwa kuandika habari za uongo juu yake kuliko kumuandika na kumdhalilisha mama yake kwa habari za uongo.
‘Niko radhi kwenda jela kama itatokea kwa mtu yoyote yule akimdhalilisha mama yangu kwani nitamfanya kitu kibaya ambacho kitanifanya nishtakiwe na nipelekwe jela ni bora unichezee mimi kuliko mama yangu ni kila kitu kwangu sipendi mama yangu apate shida,alisema Diamond.
Pia alipoulizwa katika maisha yake aliwahi kwenda kwa mganga alisema kuwa hajawahi na kwamba haamini ushirikina na anamwamini Mwenyezi Mungu.

1 comment:

Anonymous said...

wanaume mna vituko hutaki binadamu wamdhalilishe mama yako lakini uko tayari kudhalilisha wanawake wengine? jiulize hao wanawake unaowatukana kwenye mahojiano yako na wao ni wanawake kama mama yako weka heshima kwao basi kama kweli wewe ni mtu unayemuheshimu mama yako na wanawake wote kwa ujumla