ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, November 14, 2013

WEMA AWAJIBU BONGO MOVIES WALIOSUSA KUMZIKA BABA YAKE

STAA wa filamu za Kibongo,Wema Sepetu kupitia kipindi chake cha In My Shoes kinachorushwa kupitia runinga ya EATV amewajibu wasanii wenzake ambao walisusa kwenda kwenye mazishi ya marehemu baba yake Mzee Abraham Sepetu kwa kuwa yeye huwa haendi kwenye misiba ya wenzake.
Wema alisema kuwa imeshatokea baba yake amefariki na waliacha kwenda ni wao na hata wangekwenda wasingebadilisha kitu na asingerudi na kuwashukuru baadhi ya wasanii waliojitokeza kwa wingi kumfariji katika mziba huo mzito kwake.
‘Mi nawashukuru wasanii wote waliokuja kwenye msiba wa baba yangu tena ni wengi kuliko wale waliosusa ni wao hata wangekuja wasingebadilisha chochote,’alisema Wema.
Aliwashukuru zaidi wasanii waliojitolea kwa hali na mali kama Dr.Cheni,JB,Kajala,Jackline Wolper,Batuli na wengineo.
Balozi Abraham Isaac Sepetu alifariki dunia katika hospitali ya TMJ alikokuwa amelazwa akitibiwa ugonjwa wa Kisukari na kiharusi alioupata mjini Zanzibar.
Balozi Sepetu hadi anapatwa na ugonjwa na hatimaye mauti, alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji wa Vitega Uchumi Zanzibar.

Balozi Issac Abraham Sepetu,alizikwa Oct.30 kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya Magharibi Unguja.

3 comments:

Anonymous said...

pole sana wema na kwakweli umesema ukweli lakini acha maringo jamani duniani tunapita kwa nini huendi mazikoni mwa wenzako au ndo unajiona too expensive na mzuri if so thats so childish badilika mummy hata kama watu hao wasiokuja hawawezi kubadilisha kitu lakini katika kupata umaarufu wako lazima ujuwe kudeal na watu na kuwa mstaarabu other wise rudia tena shule ujuwe wenzako majuu wasanii jinsi wanavyo jua kusema on public their talk shows sawa mummy ushauri wa bure badilika mummy dunia hii si ya kufanyia mchezo mchezo kuwa muungwana mtoto wa kizanzibari

Anonymous said...

sijajua baba yake wema alikuwa mkiristo nilidhani muislamu kama yeye na wala hajawahi kuliongelea hili hata siku mmoja its not an issue ila nimeshanga kuona mipicha ya misaraba. rip mzee wetu bwana ametoa na kutoa na kakupenda zaidi

Anonymous said...

kumbe wema mzanzibari wa kimisheni mbona haajafunguka kwa hili kuwa open tukujuwe zaidi wema sepetu na pole kwa kufiwa na baba sasa itabidi uolewe ili mama naye aone wajuku wake okay baby doll