Sharon Pownall akiwa na mumewe Dylan. Tukio hilo lililogusa hisia za watu wengi lilitokea hivi karibuni mjini hapa, lilifanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Ngurudoto na kuhudhuriwa na mamia ya watu.Kwa mujibu wa chanzo makini kilichohudhuria harusi hiyo iliyofungwa kanisani, kulikuwa na kikundi cha watu ambacho hakikupenda kuona miss huyo akiolewa kiliisengenya ndoa hiyo.
“Kuna kikundi cha watu kilikuwa hakipendi kuona Sharon anaolewa hivyo kilikuwa kikipambana chinichini kuhakikisha ndoa hiyo haifungwi lakini bahati mbaya kimeshindwa,” kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo, pamoja na kampeni hizo za kuvuruga ndoa hiyo, kwa upande wake Sharon alimshukuru Mungu kwa kufanikisha ndoa hiyo aliyokuwa akiisubiri kwa hamu.


No comments:
Post a Comment