ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, November 26, 2013

Foleni Yasababisha Mh.Mohammed Dewji Kupanda Boda Boda …

Kwa jinsi inavyoonekana hapa jijini Dar-Es-Salaam, kila kukicha foleni kama inaongezeka na imekuwa ikileta kero sana kwa wakazi wa jiji hili ambapo mambo mengi huwa hayaendi kama inavyotakiwa kutokana na wakazi kushindwa kufika maeneo ya mipango yao katika muda muafaka. Na hii hali ya foleni ya jiji la Dar husababishwa na kuongezeka kwa magari mengi na pia kuwa na barabara finyu ambapo ikitokea hali ya mvua kidogo tu basi hali ndo inazidi kuwa mbaya.
Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter leo, Mheshimiwa na mfanyabiashara mkubwa jijini Dar Bw. Mohamed Dewji alitoa malalamiko yake katika akaunti yake ya twitter kuwa anahitaji kuwa na Helicopter ili aweze kuwahi na kuepuka foleni ya jiji la Dar. Na hii hapa chini ndiyo kauli aliyotoa Mheshimiwa huyo baada ya kulazimika kupanda usafiri aina ya Boda Boda ili asichelewe kufika katika mkutano ambao alitakiwa kuhudhuria

3 comments:

Anonymous said...

I thought barabara hufungwa wanapopita waheshimiwa huko Bongo. The Hon Dewji needs to man up and face the reality of the country.

Anonymous said...

That's what you get when you sit in the parliament like a cheerleader. Tanzania is moving backward from Ikarus kumbakumba to bodaboda.

Anonymous said...

Tatizo ni pale VIONGOZI ambao sisi wanyonge tunawategemea nao wanajichanganya kwenye kundi la KULALAMIKIA HALI HII. Ukiona wewe ni kiongozi na unaishia kulalama tuu, tambua UONGOZI umekushinda maana WANYONGE hawataki kusikia kilio cha wenye KUTAKIWA KUTATUA matatizo yanayowakabili.