Wednesday, November 20, 2013

KISOMO CHA MAREHEMU MAMA HAWA HAJI KAMANGA KESHO JMOSI HOUSTON

Marehemu Hawa Haji Kamanga
Kisomo cha kumuombea Mama Hawa Haji Kamanga kitafanyika kesho (Jumamosi 11/23) kwenye msikiti wa MASJID EXPO uliopo kwenye kona ya Westheimer na Hayes. Msikiti upo kwenye shopping center ya Fitness Connection. Kisomo kitaanza saa kumi na moja jioni (5:00 pm).

Mara baada ya kisomo cha msikitini shughuli itahamia Ukumbi wa Safari kwa ajili ya chakula na vinywaji kuanzia  saa kumi na mbili jioni mpaka saa tatu usiku (6pm to 9pm).

Anwani ya Safari ni 7601 De Moss Dr, Houston, TX 77036. Tunaomba Vyakula na vinywaji vipelekwe moja kwa moja ukumbini Safari.



Asanteni

2 comments:

Anonymous said...

Kaela Mama ako alikuwa anakusifia kwa jitihada Zako zakisaidia pale nyumbani .mungu akubariki mwanangu akupe moyo wa kujua amepumzita

Anonymous said...

Huyu mama alikuwa jirani yetu pale upanga .Huyo kaela alikuwa anamsifia ,kaela mimi sikujui ila mama ako ulimtunza duh !!! Mungu akubariki uwatunze na uwaongoze ndugu Zako .maana wewe ndio ulikuwa tegemeo la mama kamanga .Nina Imani umekuja kumsindikiza njia ya milele .Anepumzika yupo kwa mungu .mungu awabariki watoto wa mzee marehemu kamanga mkae kwa Amani .RIP mrs Kamanga