Kumbukumbu mbaya pia ni sababu nyingine inayochangia wanawake wengi kupoteza hamu ya tendo. Wanawake waliowahi kubakwa au kunyanyaswa sana na wapenzi wao, hupoteza kabisa hamu ya kukutana kimwili hata kama watakutana na wapenzi wapya ambao hawahusiki kabisa na matatizo yao ya awali.
Sababu nyingine ni pamoja na uchovu wa kazi, mawazo, kushiriki sana tendo la ndoa na kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja (usagaji).
NAMNA YA KUKABILIANA NA TATIZO
Pata usingizi wa kutosha
Endapo unasumbuliwa na tatizo hili, jitahidi kupata usingizi wa kutosha kila siku. Fanya mazoezi mepesi kabla ya kulala kisha panda kitandani mapema. Lala angalau kwa saa nane kila siku, utaona mabadiliko.
Pambana na msongo wa mawazo
Usiruhusu msongo wa mawazo ukutawale, fanya mazoezi ya kuondoa msongo kama Yoga, tahajudi na masaji ya mwili mzima. Pendelea kufanya mambo unayoyapenda ili kuondoa msongo.
Vyakula
Kuna vyakula ambavyo vikitumiwa, husaidia kuamsha hisia na hamu ya kushiriki tendo la ndoa. Mwanamke mwenye tatizo hili anashauriwa kuvitumia vyakula hivyo ambavyo tumewahi kuvitaja kwenye matoleo yaliyopita.
Zungumza na mwenzi wako
Pia wanawake wanashauriwa kuzungumza na wenzi wao na kuwaeleza juu ya tatizo hili kisha wawaeleze wakifanyiwa kitu gani watajisikia hamu ya tendo. Wanaume ambao wake zao wana tatizo hili, wanashauriwa kutumia muda mrefu kuwaandaa wenzi wao kihisia kabla ya tendo.
GPL
No comments:
Post a Comment