ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, November 14, 2013

Kutoka Facebook : Kama ligi kuu ya England ingekuwa darasa, je mambo yangekuwa hivi?


Kwenye pitapita yangu facebook nimekutana na post kadhaa na hii ni moja ya post iliyonivutia na kujiuliza kama ligi kuu ya England ingekuwa darasa kweli mambo yangekuwa hivi
1. MANCHESTER UNITED ni mwanafunzi wa kawaida tu darasani, hua hapendi kujionesha kama ana akili ila anapendwa sana na waalimu kwa sababu hujituma sana katika mitihani ya mwisho na mara nyingi hutoka wa kwanza. Wengine hudhani hua anaoneshwa mitihani na wasimamizi. Hta hivo mwalimu mkuu amehama shule sasa kuna wasiwasi maendeleo yake darasani yakazorota siku zijazo.

2. LIVERPOOL ni mtoto aliyekua na akili nyingi lakini kipindi hiki hafanyi tena vizuri darasani ila mafanikio aliyoyapata huko nyuma yametunzwa vizuri ofisini za mwalimu mkuu na ukibishana nae anakuelekeza uende ofisi kuu kuangalia matokeo yake ya nyuma. Lakini anaonekana kujitahidi sana kukesha ili aweze kurudia mafanikio yaliyokua yamemzunguka japo sasa hivi uwezo wake wa kuelewa si mkubwa kama zamani

3. MANCHESTER CITY ni toto la tajiri ambalo hununua vitabu vya bei ya juu lakini hua havisomi na vingine huishia kuwaazima wengine.

4. ARSENAL ni mvulana aliyekua akiitwa jiniasi na mwenye mwandiko mzuri kuliko wote shuleni lakini ameanguka sana kimasomo baada ya kuanza kuuza vitabu vyake akidai atanunua vizuri zaidi hivi karibuni. Pesa alizouzia vitabu ameziweka chini ya mto na kila anazichungulia hutabasamu na kujisikia raha.

5. TOTTENHAM HOTSPUR huyu ni mtoto ambaye yeye hufanya vizuri kwenye somo moja tu. Mara zote hujaribu kushindana na jirani yake anaye kaa dawati moja naye Arsenal ingawa hajawahi kufanikiwa.

6. CHELSEA ni mtoto anayepewa kila kitu anachohitaji shuleni na hudekezwa sana
hufanya vizuri anapopewa anachotaka ila anapofeli humsemea mwalimu wake kwa baba yake kuwa mwalimu ndio tatizo na baba humletea mwalimu mpya mara moja. Na Ayo...

No comments: