ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, November 13, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILA AIFARIJI FAMILIA YA MAREHEMU MUSSA SAMIZI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika Kitabu cha maombolezo ya marehemu, Mussa Samizi, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Tegete jijini Dar es Salaam, leo mchana kwa ajili ya kutoa pole. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mke wa marehemu, Mussa Samizi, Bi. Misingo Samizi, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Tegeta jijini Dar es Salaam, leo mchana. Marehemu Samizi alikuwa ni Mtumishi Mstaafu wa Umma,aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika Chama cha Mapinduzi CCM na Serikali. Marehemu anazikwa leo jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

1 comment:

Anonymous said...

Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amin