RAIS wa Malawi, Joyce Banda ametajwa kuendeleza chokochoko baina ya nchi yake na Tanzania, huku sasa akidaiwa kutumia redio na runinga za nchini mwake kutangaza kuwa mkoa wa Ruvuma, viongozi na wananchi wa ukanda wa Ziwa Nyasa ni mali yake.
Aidha, amesitisha safari za meli ya mv Ilala iliyokuwa ikifanya safari kwenye Ziwa Nyasa kusafirisha mazao na wananchi wa ukanda huo upande wa Tanzania.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa soka wa Mbambabay jana, Mbunge wa Mbinga Magharibi, John Komba, alisema Rais Banda ambaye aliibua upya mzozo wa mpaka baina ya nchi hizi mbili, kuwa ni mkorofi kutokana na kufanya vitendo vinavyoonesha uhusiano baina ya nchi hizi mbili kuzorota.
Komba alibainisha vitendo hivyo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akisema imefika mahali Rais Banda anapotosha ukweli kuhusu mpaka kati ya nchi hizo mbili na kudai sehemu ya mwambao wa Ziwa upande wa Tanzania ni yake.
Mbunge huyo alisema jimbo la Mbinga Magharibi ambalo ni Wilaya ya Nyasa, wanasikiliza matangazo ya redio za Malawi, na anazitumia kupotosha umma kuwa ukanda wa Ziwa Nyasa ni mali yake na wananchi wanaamini hivyo.
Rais Banda anatangaza kupitia vyombo vya habari vya nchi yake ambavyo vinasikika vizuri katika wilaya hiyo kutokana na wilaya ya Nyasa kutopata mawasiliano ya redio na runinga za nchini. Komba alisema kutokana na wilaya hiyo kukosa mawasiliano ya vyombo vya habari, wananchi wake wanakosa kusikiliza matangazo zikiwamo hotuba za viongozi wa Taifa.
Wananchi wanakosa kusikiliza matangazo zikiwamo hotuba ya Rais Kikwete ya kila mwezi na hotuba za viongozi wengine wa kitaifa wakiwamo Makamu wa Rais na Waziri Mkuu.
“Kutokana na kukosekana usikivu huo, Rais Banda anatumia nafasi hiyo kutangaza kuwa viongozi wote wa wilaya na mkoa na eneo lote ni mali yake,” alisisitiza Komba. Aliongeza kwamba watu wote walioko kwenye mkutano huo isipokuwa Katibu Mkuu Kinana, akiwamo Dk Asha-Rose Migiro ambaye alizaliwa Mbambabay wote ni mali ya Rais Banda.
Mbunge huyo alisema wananchi wa eneo hili nao ni Watanzania wanaostahili kusikia na kupata habari za nchi yao, badala ya kusikiliza nyimbo na matangazo ya Malawi ambayo yanakuwa na ajenda zake.
Mbunge Komba alimwomba Katibu Mkuu Kinana kwenda kuhimiza kutekelezwa haraka kwa ahadi ya Rais Jakaya Kikwete ya kuleta meli ili kuwa na usafiri wa uhakika wa mali na wananchi katika eneo hilo.
Kinana alisema ahadi ya meli ya Rais, hiyo ana uhakika itatekelezwa na kufafanua kuwa meli tatu zinatengenezwa Korea Kusini na zitakapokamilika ya Ziwa Nyasa itapelekwa kutoa huduma.
Alisema baada ya Banda kuondoa meli hiyo wananchi wa Mbambabay wanatumia boti dogo kusafirisha abiria na mizigo, hali ambayo inatia shaka.
Kinana alisema amesikia kilio cha Mbunge Komba, kwamba ahadi ya Kikwete itatekelezwa ili kuwapa wananchi usafiri wa meli, ingawa itatumia muda kutokana na kuhitaji muda mwingi kubuni na kutengeneza
4 comments:
Wanawake kwa uizii tu ndo wenyewe! Ndo maana sipendi nchi zinazomilikwa na mwanamke Kama UK na nyingineee!
Je kuna wanawake waliokulea wewe? na hao walikufunza wizi? kama ulilelewa na wanaume tu unahaki hiyo ila kama ulinyonyeshwa kwa upendo na mwanamke au hata kupewa malezi basi inabidi uwe na heshima. sio tu kuongea bila kufikiria. Maana hapo inaonyesha uelewa wako wa maendeleo ya kijamii. wewe unakua mjinga kuliko huyo mama anayedai tanzania nayo ni mali yake. Usiwadharau wanawake hata shule wewe hukwenda inaelekea maana hata walimu wa shule ya msingi walikua wanawake lol
behind any successful man lies a woman so jamaa hana mkee wala hana ndugu wa kike wala mama muacheni kamaa alivyo dunia itakuja kumfunza na atastaarabika na kuwa na heshima na wanawake naona aliteswa sana na wanawake huyu toka kulelewa kwake mpaka hapo alipo si bure
si kweli wanaume ndo wezi kuzidi wanawake na kila balaa la duniani mwanamme amelianzisha,uk nani anamiliki ile nchi karisi kutoka kwa wazazi wake na ndo maana yeye ni queen lakini si waziri mkuu ndo anayoendesha.
kuwa mstaarabu bwana tena muombe mungu wako samahani kwa sababu yeye ndo aliyewaumbwa hao wanawake na wewe kuwa mwanamme so usimkose mungu wango ukaja ukalaanika bure kwa comment za kijinga jinga kuwa mstaarabu bwana
nadhani wewe pia ni mwizi mkubwa umejuaje wanawake wezi kama wewe huna tabia za wizi tupe data na research zako siyo chuki zako juu ya wanawake kuwa mwana uione dunia
Post a Comment