Ndugu Wana CCM na Watanzania wote!
Yah: Mkutano wa Tawi la CCM New York Metro (New York na Tri-State area PA, NJ & Ma)
Tunapenda kuwakumbusha tena kwamba Tawi letu la CCM hapa lilifunguliwa rasmi Agosti 25, 2012 na Mh. Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM-Taifa.
Mkutano wa Wanachama wote ni Jumapili saa nane na nusu mchana (2:30 pm)Novemba 17, 2013.
Mahali: 2031 Adam Clayton Powell Blvd.(7th Ave. Between 121st and 122nd) Harlem, New York.
Mkutano huo utanogeshwa na msanii mahiri kutoka Tanzania Mwana FA. Usikose come one come all.
Tutakuwa na burudani ya muziki pamoja na karamu maalum kwa wahudhuriaji wote.
Tutakuwa na burudani ya muziki pamoja na karamu maalum kwa wahudhuriaji wote.
Tunaomba yeyote anaependa kujiunga na Chama au ni Mwanachama tayari wasiliana nakamati maalum.
1. Isaac Kibodya - Tel.(413)219-1153
2. Prof. Kamazima Lwiza - Tel.(631)278-3859
Email: ccm.grassrootsny1@gmail.com
Kidumu Chama Cha Mapinduzi!







11 comments:
tunajua ni kinyume cha sheria juihusisha na vyama vya siasa hapa u.s.a nawapigia uhamiaji na police kutoa ripoti,ngoja mrudishwe bongo mkaishabikie vizuri ccm
hahahaha
WaTanzania hatujui tuendako tukiwa huku ughaibuni. Tunashabikia vyama ambavyo siku ya kupiga kura huna haki ya kupiga kura!!, Badala ya kutafuta na ukweli wa dual citizenship tunajibandika mibendera ya kijani Marekani kote! Mliwaona Wamarekani wakipeperusha bendera kule nyumbani na popote pale, japokuwa wana haki ya kupiga kura wakiwa nje ya nchi yao!. Tufikirie mambo mengine ya maana tuachane na ulimbukeni wa siasa uchwara zinazolenga kuwanyamazisha wasemaji wa haki za walio wengi. Tuwe wamoja kusaidia vizazi vya taifa lijalo sivyo tutabakia na taifa mbumbumbu na ulaji na wasio na elimu sana miaka 20 ijayo!!. Asante.
Mdau ulichosema ni kweli. Form za green card na uraia zinauliza kama ulishawahi kujihusisha na cham cha kisoshalisti. Mbona wataigomea CCM ili wasipiogwe chini.
hahhaha !!!!wewe piga polie na uwamiaji utashangaa wewe ndiyo kwanza unarudi nyumbani chezea chama tawala wewe jaribu uwe mfano kidumu ccm
basi subirini si mnajidai wajanja basi ngojeni na wengi wenu hamna makaratasi mnasaidiwa na chama au mnataka kutoka kwenye vyama msaidiwe subirini si mnajidai wajanja subirini msije mkalia tu bure wengi tunakujuweni hamna makaratais mnajidai kutamba na vyama mchwarwa subirini chungu kinawivya kila mmoja atagongewa mlango wake kwenye geto lake au anapofanya kazi kwa mchini cannal street na vijimkavu
namependa kweli alivyonena mdau wa pili katika hapo juu kwenye comment zake amesema kweli na kweli kaani mkitafakari jamani tusiwe wavivu wa kupapanua mambo tusiwe wafikiriwa na kubruzwa ovyo na vyama hivi tuwe wafikiri jamani tuzingatiiye maneno ya mdau wa pili ni kweli tupu amenena jamani tuko ncho za watu jamani maisha yanakwenda hayarudi nyuma na tunakuwa na nguvu kuna siku zitatuisha tujenge maisha yetu badala ya kushabikia vyama hivi jamani tufikiriye mbali jamani nakuombeni ndugu zangu watanzania wote wakike kwa wakiume jamani please jamaa amenene kweli tupu mungu ambariki kwa maneno yake amen
Hongera chama kimeshika hatamu....lakini tusipuuze ushauri, viongozi fuatilinie vibali ni makosa kuendesha shuhuli za kisiasa bila kibali nchini Marekani na tukivamiwa wengi hatuna paper na huyo jamaa wa kwanza ameshasema atapiga cim polisi au uhamiaji.halafu nimeshangwazwa na hao wanachama wapya hao wazazi wao ni watumishi wa serikali ya ccm lakini ndio wanaingia leo CCM?walikuwa chama gani au ndio hivyo tupige kelele sisi watoto wa makapuku watoto wa wakubwa hata kadi hawana
mimi sintokuja na nawasihi wenzangu wasiokuwa na paper wasije hawa jamaa watatuletea uhamiaji bure
Yaani New York majungu yatawashinda hapo mmeshaanza kuleta chuki zenu binafsi! Sio mara ya kwanza humu Vijimambo tunaona mikutano/sherehe za CCM states mbalimabali leo New York wameamua waosha vinywa wameanza kauli ambazo hazina mbele wala nyuma doh! mnafikia mpaka kusema mtaenda kusemeana makaratasi really? unatokwa na roho kuona watu wamevaa magwanda ya kijani? yaani mtaacha lini unafki wa kipumbavu?
Kidumu chama cha mapunduzi oyee my mnanikumbusha mbali sana tangu enzi za ujana wangu
Post a Comment