Wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Lady Jaydee (kushoto) akiimba sambamba na Professa Jay katika tamasha la burudani lililofanyika katika viwanja vya Leadars Club Kinondoni |
Mwanamuziki wa kundi la P square, Peter Okoye, akitoa burudani ya aina yake kwa maelfu ya Mashabiki waliojitokeza katika viwanja vya leaders club, Tamasha hilo lilidhaminiwa na Vodacom Tanzania burudani hiyo ya karne ilitolewa kwa mashabiki wa muziki pale leaders club.
Mwanamuziki wa kundi la P square, Peter Okoye, akionesha uwezo wa kulimudu gitaa tofauti na kuimba tu, wakati wa tamasha la burudani lililofanyika katika viwanja vya leaders club, Wasanii hao mapacha walikonga nyoyo za maelfu ya mashabiki waliojitokeza katika Tamasha hilo lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Mashabiki waliojitokeza katika tamsha la wasanii kutoka nchini Nigeria
Msanii Judith Wambura, Lady jay dee akiteta jambo na wasanii wa musiki wa kundi la P-Square kabla hawajapanda jukwani na kutoa burudani kali kwa maelfu ya mashabiki waliojitokeza katika Tamasha hilo lililofanyika viwanja vya leaders club na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania
Dar es Salaam, 24 Nov 2013 . . Siku ya jumamosi mwezi huu pale leaders club ilikuwa Usiku ya kihistoria kwa tasnia ya burudani nchini Tanzania baada ya wasanii mapacha wa kundi la P Square, Peter na Paul Okoye kutoa burudani ya aina yake ambayo haijapata kutokea kwa muda mrefu hapa nchini kwa maelfu ya mashabiki wa burudani waliojitokeza katika viwanja vya leaders club.
Wakiwa ni wasanii wanaokonga nyoyo za mashabiki wa muzikini barani Afrika walisindikizwa na wasanii kutoka hapa nchini ambapo jukwaa lilifunguliwa na msanii Ben Pol ambaye alikonga nyoyo za mashabiki wa muziki kwa kuimba kwa muziki wa bendi uliokuwa ukipigwa live na bendi ya machozi bendi.
Huku hamu ya mashabiki wa burudani ikianza kukolea kazi iliyofanywa vyema na mwanadada Rady Jay dee iliwatoa jasho mashabiki waliofurika katika viwanja hivyo, huku akiimba wimbo wa joto hasira uliopokelewa vyema na mashabiki ulimshuhudia Profesar Jay akipanda jukwaani huku akichana sehemu ya wimbo huo alioshirikishwa na mwanadada Anaconda.
Kazi ya burudani kwa wasanii wa Tanzania ilifungwa vilivyo na msanii Jo Makini au mwamba wa kaskazini alie limudu jukwaa na kuwapagawisha vilivyo mashabiki wa muziki huku akisaidiwa vyema na msanii mwenzake Niki wa Pili ambao kwa wasasa wanatamba na kibao chao cha tatizo ni bei ya mkaa kilicho pokelewa vyema na mashabiki wao.
Ulifika wakati ambao ulitarajiwa na maelfu wa mashabiki waliojitokea katika viwanja vya leaders club ambapo wasanii Peter na paul okoye, walipopanda jukwaani na kuanza kutoa burudani kwa mashabiki. Wasanii hao walianza kwa kuwashukuru mashabiki waliojitokeza na kuishukuru kampuni ya Vodacom kwa kufanisha ujio wao hapa nchi.
P Squre walitoa burudani ya kipekee kwa muda wa masaa mawili mfurulizo bila ya kuchoka na kila walipoweka kibao kingine ndipo moto wa mashabiki ulizidi kuwaka na kukidhi vilivyo kiu ya mashabiki wa burudani.
Burudani ya kipekee ilikuwa pale ambapo wasanii hao walianza kuonesha vipaji tofauti walivyonavyo, huku Peter akionesha uwezo wa kupiga gitaa vilivyo alijibiwa na kaka yake Paul akijibu mapigo kwa kupiga vilivyo ngoma huku wakipokea shangwe kutoka kwa mashabiki wao.
Shukurani za kipekee kwa kampuni ya Vodacom Tanzania iliyofanikisha ujio wa wasanii hawa waliotoa burudani ya kipekee kwa Watanzania hakika itakuwa ni historia ya aina yake kwa tasnia ya burudani na fundisho kwa wasanii wa hapa nchini.
No comments:
Post a Comment