ANGALIA LIVE NEWS

Friday, November 29, 2013

PENYE UMATE MATE HAKUNA KINACHOSHINDIKANA MBWAI MBWAI TUU MKE ANUNUA TARAKA KWA M.4

Mohamed Kismati akimvisha pete mkewe Rukia Apach siku ya ndoa yao.
Ndoa hiyo ilifungwa miaka miwili iliyopita na kufuatiwa na sherehe ya kifahari katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar mwaka juzi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wawili hao wameachana kwa madai kwamba baba mkwe wa Rukia kukataa mkwewe huyo afanye kazi zaidi ya kuwa mama wa nyumbani.
Wanandoa hao wakikata keki siku ya harusi yao.
Akizungumza na Ijumaa, Rukia alisema kwamba mumewe alimuahidi kumwendeleza kielimu wakati alipokuwa akisoma kidato cha sita pindi akimuoa.
“Awali mume wangu aliniahidi kuniendelea kimasomo, lakini baada ya kuolewa nikakataliwa hata kufanya kazi, amri ambayo ilitolewa na baba mkwe wangu ambaye ni mfanyabiashara,” alisema Rukia.
Wazazi wa bwana harusi. Kulia ni mkwe wa Rukia alliyemzuia kufanya kazi.
Mwanamke huyo alidai kwamba familia ya mumewe ilishikilia msimamo huo hadi ndoa yao ilipovunjika hivi karibuni.
Kama vile haitoshi, Rukia amedai kuwa alilazimika kulipa baadhi ya vitu na kutoa kiasi cha shilingi milioni 4 ili aweze kupewa talaka yake.
Rukia alidai kwamba chanzo cha yote kilianza baada ya baba mkwe wake kwenda Dubai kuangalia biashara zake, naye kuutumia mwanya huo kumuomba ruhusa mumewe ili akafanye kazi na kukubaliana ndipo alipoanza kazi Mlimani City, jijini Dar.
Maharusi katikati wakiwa katika picha ya pamoja na wazazi wa bibi harusi (kushoto) na wazazi wa bwana harusi (kulia).
Hata hivyo, baba mkwe aliporeja akakipinga kitendo hicho na kumwambia mwanaye kwamba kumruhusu mkewe kufanya kazi ni sawa na kumtoa sadaka kwa wanaume wengine.
“Niliomba ruhusa ya siku tatu kazini ili nipate muda wa kuzungumza hilo na mume wangu lakini ilishindikana, nikaamua kurudi kazini,” aliendelea kusema Rukia.
Maharusi hao katika pozi.

Mwanamke huyo alisema kwamba baada ya kurudi kazini, familia ya mumewe ilimnunia na kumtaka kuondoka huku wakimzuia kuingia chumbani kwake.

“Waliniambia mizigo yangu wataniletea, nikaondoka na kurudi kwetu,”alisema Rukia kwa majonzi.
Pamoja na familia hizo kukutana na kulizungumzia jambo hilo, lakini mwafaka ulishindika ndipo upande wa mumewe ulipodai kulipwa shilingi milioni 7 kama gharama za mahari yao ili watoe talaka.

“Sikuolewa kwa pesa hizo, tukalifikisha suala hilo Bakwata (Baraza Kuu la Waislamu Tanzania) na kukubaliana kuwalipa shilingi milioni 4 hivyo ikawa kama nimeinunua talaka yangu,” alisema Rukia.

Mume wa Rukia, Mohamed alikiri kutokea kwa jambo hilo na kusisitiza kuwa alimuoa mwanamke huyo na hivyo alipaswa kufuata matakwa yake, vinginevyo ndiyo sababu kubwa ya kumuacha.

Familia hizo zilikutana Bakwata Jumatatu iliyopita na Rukia akakabidhiwa vitu vyake alivyoviacha kwa mumewe pamoja na pete ya ndoa.

Tafrani ilizuka baada ya mama mkwe kudai arejeshewe pete aliyovikwa mke huyo siku ya harusi, akimwakilisha mwanaye ambaye hakuhudhuria kikao hicho.

Shehe wa Bakatwa (jina halikupatikana) aliwataka kukubaliana na aya ya 20 katika Surat Nisai ambayo inakataza kumdai mali yoyote ile uliyomzawadia mkeo.
“Mlioana kwa hisani na muachane kwa hisani isitoshe unapomuacha umeshamtumia si vyema kumdai mali uliyotoa,” alisema shehe huyo.

4 comments:

Anonymous said...

upuuzi wa huo utamaduni, wakati serikali inasisitiza watanzania wafanye kazi kwa bidii, wengine wanataka binadamu wengine wasifanye kazi....kisa kuwa ataonana na wanaume! Kuna watu wengine humu duniani wana matatizo ya akili, wanachowaza ni ngono tu, kwa mtaji huu tutabaki nyuma na wengine wetu wa east Africa watatupita kama tumesimama kwa sababu ya wajinga walioko nchini mwetu wenye mawazo mgando.

Anonymous said...

Bibie yu atakiwa abakie nyumbani tayari tayari kumstarehesha bwana ati. Huku akitengenezea bwana manhunjumati kama vile machapati,marosoroso na urojo atii babu...teh teh

Sio kukicha mwanamke huku kule kukuru kakara na njia kutwaaa. Si mnatujua si pande wa kuleee Mchambawima:-)

Anonymous said...

Ni TALAKA na sio TARAKA

Anonymous said...

Hata mimi kama nina pesa sioni sababu mke wangu akaajiriwe kwa mshahara wa laki3 kuuza duka mlimani, nitamuona wa maana kama ataniambia anata kufungua biashara yake, kama alikua ana elimu kubwa sawa najua elimu yake sitopenda iende bure lakini siyo amemaliza form IV akauze duka hiyo kazi au mnatafuta matatizo.