
Mwanamuziki gwiji la Afrika aliyetamba enzi hizo Tabu Ley Rocherou amefariki leo asubuhi nchini Ubeligiji alipokuwa akiishi. Mwanamuziki huyu raia wa DRC alikua akiugua kwa muda mrefu akisumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi. Tabu Ley alizaliwa mwaka 1940 tarehe 13, mwezi Novemba.
Tabu Ley alikuwa ni muasisi na kiongozi wa bendi ya Orchestre Afrisa International akishirikiana na mkung'utaji wa gitaa gwiji Dr. Niko, Bendi iliyotamba sana enzi hizo alikuwa ni mmoja ya mwanamuziki aliyevumbua vipati vya wanamuziki wengi wakiwemo Mbilia Bel na mpiga gitaa maarufu Lokassa ya Mbongo ambaye alianzia kwake miaka ya 1960 na yeye ndiye aliyempa jina hilo.
2 comments:
RIP Tabu Ley, marehemu baba yangu alikuwa akizipenda sana nyimbo zako.Nakumbuka nilipokuwa mdogo kama sikosei ilikuwa mwaka 1987 Tabu Ley na Mbilia bel walikuja kutumbuiza Tanzania baba yangu akahakikisha tunapata mkanda wa video, tukawa tukiangalia nyumbani mpaka na sie watoto tukaanza kuwapenda.Pumzika kwa amani mzee Rocherou.
muzina. RIP tabu ley
Post a Comment