ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, November 5, 2013

Yahusu Kuwashukuruni wote

Wapendwa,
Mwenyekiti,
Baraza la wazee
Wanawake wote
Kamati ya maandalizi ya mavuno,
Washarika wote.

Salaam za upendo, furaha na amani ziwafikieni wote mahali popote mlipo!

Wahenga walisema "Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu" Usemi huu umetimia vema katika jitihada mbalimbali ambazo tumekuwa tukizichukua kufanya kazi ya Mungu muda wote na hata kutuwezesha kufikia tulipofika.Mungu na ashukuriwe sana!

Nitumie nafasi hii kusema usemi huo pia umetimia kwetu kwa jinsi tulivyoshirikiana wote kuwezesha kufanikisha sikukuu ya mavuno. Napenda niwashukuru sana kutoka mtu mmoja mmoja katika kila jambo na kila kitu alichohusika nacho katika maandalizi ya mavuno hadi kufikisha siku ya jana kuwa na mafanikio mazuri.Mungu awabariki sana.

Ni maombi yangu mbele ya Mungu kwamba, Mungu aendelee kutupa na kutuimarishia UMOJA wetu huu na mshikamano pasipo kitu au mtu yeyote kututenganisha kama Wimbo wa Kwaya yetu ulivyoimbwa kwa wimbo Maalumu wa mavuno.

Mmbarikiwe sana!

Rev. Andrea Mwalilino
Minnesota Swahili Christian Congregation
2730 E 31st Street
Minneapolis, MN 55406

No comments: