STORI kuhusu maisha ya mama mzazi wa staa wa komedi Bongo, marehemu Husein Mkiety ‘Sharo Milionea’, baada ya kifo cha mwanaye huyo imemliza Rich Mavoko ambaye alikwenda kumtembelea nyumbani kwake kijijini Lusanga, Muheza mkoani Tanga.
Rich Mavoko akifuta machozi alipomtembelea Mama Sharo Milionea.
Akiteta machache na Risasi Vibes, Mavoko alisema, yeye kama msanii aliguswa kwenda kumsalimia mama Sharo kwa kuwa wote ni wasanii na aliona mama huyo anahitaji faraja kutoka kwa watu waliokuwa karibu na mwanaye.
“Mama alifurahi sana kuniona. Tulizungumza mengi lakini niliguswa sana na matatizo aliyonayo mama yetu. Mama anasema, mali nyingi za marehemu mwanaye, amekuwa akizisikia tu lakini hajapewa.
Mavoko na Mama Sharo wakiwa katika kaburi la Marehemu Sharo Milionea.
“Kiukweli mama Sharo anatia huruma sana kwani faraja imepotea, mali za mwanaye hazioni, amebaki akitia huruma.
Unajua marehemu alikuwa akimsadia sana mama yake, ndiyo lilikuwa tegemeo lake kubwa. Ameondoka na kumuacha akiwa hana la kufanya, mbaya zaidi hata mali zake ambazo zingepaswa kumsaidia kipindi hiki, wajanja wamezidhulumu.
“Dunia haina usawa kabisa. Kiukweli inatia huruma sana. Nawasihi wasanii wenzangu na wadau wa sanaa, inatakiwa tukumbuke wenzetu waliotangulia tena kwa kuwaenzi kwa kila njia.Kuna vitu vinauma sana amenieleza tangu kifo cha mwanaye haki zake nyingi hajui zilipo. Tuungane wasanii tuwasaidie wazazi wa wasanii wanaotangulia mbele za haki,” alisema Mavoko.
GPL


2 comments:
Luke wacha kujitoa fahamu kwa kuweka huu upupu wa kule Bongo maana una vitu vingi na vya maana sana vya kuposti kuliko hivi visivyo na faida yoyote kwa jamii... It's just too personal, WHY..!!?
Ni hiyari yako kuufanyia kazi huu ushauri au la..!!!
mdau wa mwanzo kuwa mstaarabu je ungekuwa wewe umeondoka dunia na mama yako anateseka je ungesemaje ungejisikiaje wewe kuwa binadamu luke big up my man na luke hafanyi kazi kwako anafanya kazi kwa jamii nzima so anahaki ya kutufahamisha na kutuelimisha na kutuburudisha watu wote wa rika lote na fani yote hata udaku pia luke tuwekee tupunguze stress jamaa akiona haina faida kwake kwetu tunayo faida kila mtu ana mtazamo wake asikulazimishe labda ndo mmoja wapo aliye kalia mali za sharoo millionea walikuwa wana mfanya punda wao wa kumchuma mpaka wammemuuwa na wao kufaidi mali zake
na wasi wasi sana na jamaa huyu atakuwa mmoja wapo asikutishe bob luke achana naye mwizi mkubwa to personal mbona tunapowekewa story zinginewe za ma staa ambazo ni to personal husemi ache zako wewe bangi peleka mwanza
Post a Comment