ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, December 17, 2013

MBUNGE AMPONDA MISS TANZANIA KWA KUTOKUJUA KUONGEA KISWAHILI

Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred hajui Kiswahili? Well, tuliowahi kukaa naye kidogo tunaweza kumtetea kuwa anakijua haswaa, sema hupendelea zaidi kuongea kimombo. Pengine ndio maana mbunge wa viti maalum kutoka Zanzibar, Rukia Ahmed anahisi mrembo huyo haijui lugha yake ya taifa.
Akiongea bungeni leo, Bi. Rukia amesema Brigitte Alfred hafai kuiwakilisha Tanzania kwakuwa hawezi kuzungumza Kiswahili. Mbunge huyo alienda mbali zaidi kwa kupendekeza mashindano ya Miss Tanzania yafutwe na badala yake yawekwe mashindano ya Sayansi kwa manufaa ya taifa.
Akijibu kauli hiyo, Brigitte amesema: Meanwhile as our county suffers from 3rd world problems this is what is being discussed bungeni. I would love to meet this this woman! Asante mama,” ameandika mrembo huyo kwenye Instagram. “All of your comments give me hope that there’s still sensibility out here,” aliongeza.
“Mh.Rukia amekosa mada bungeni?*rollingmyeyesoutloud*,” alitweet.
“Anko in the office must be jumping for joy right now-they love to say ‘I told you so’-In Kiswahili ofcourse.”
Hata hivyo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara alisema serikali haiwezi kuyafuta mashindano hayo kwakuwa yana umuhimu mkubwa kwa taifa na yamekuwa yakiitangaza nchi na shughuli za utalii.Credit:Udakuspecial

7 comments:

Anonymous said...

huyo mbunge hana akili ndio maana warembo wetu wengi hawajui kiingereza. unawauliza maswali wanakutizama na kucheka siyo wote of course.

Anonymous said...

Bado Tanzania imegubikwa na wabunge mizigo.ns hii yote nikutokana na serikali kuwapa madaraka watu bila kujua upeo wao...bali upendeleo...huyu mama hafai hata kuwa diwani wa kata ya vijibweni....Dada ysngu.Miss Tanzania...usikate tamaa..na hawa wabunge wakupachikwa..wewe ulichaguliwa na jopo la majaji...hongera

Anonymous said...

Ms Tanzania, wewe endelea kukimwaga kimombo wala usimsikilize huyu mbunge. Yeye afanye kazi aliyotumwa na wapiga kura wake (kama siyo munge wa kuteuliwa).

Anonymous said...

kwa maoni yangu wengi wa watanzania wa kizazi kipya hawajui kiswahili wala hicho kiingereza wanachohusudu kukiiga.nimewaona wengi tu wa ma miss universe wameshinda wakiwa hawajui kiingereza na waliongea kupitia mkalimani.utawaona baadhi ya wasanii wetu wengi wanatuchanganyia lugha wanapoongea, lakini inapokuja wakihojiwa kwa lugha moja kati ya mbili wanazozichanganya basi hawaongei kwa ufasaha kwa lugha yoyote kati ya hizo. mtoto wangu mmoja ambaye nilimzaa USA amepata bahati ya kuzijua kwa ufasaha lugha ya kiingereza na kiswahili mara nyingi amelibaini tatizo hili la sisi waswahili hasa wa kizazi kipya, tunaendelea kuipoteza lugha ya kiswahili kwa sababu ya kuibeza na pia wengi wetu hatujaweza kuimudu vyema lugha ya kiingereza japo tunaihusudu sana. wenzetu wa nchi jirani na tanzania wakiwa kwao wanakibeza kiswahili kama hakina manufaa yoyote, wakifika hizi nchi za ulaya na marekani wanakaa mbele kama ni wajuzi wa lugha hiyo ili kujipatia ajira za ukalimani na ufundishaji wa kiswahili.

Anonymous said...

Ndugu yangu hapo juu sema "jopo la majaji wa Ms. Tanzania" kitu ambacho sidhani hata ni muafaka kuwaita jopo la majaji kwa sababu tunaposema jopo la majaji tunamaanisha majaji wa mahakama kama sijakosea.
Back to the issue, mi sioni sababu ya Ms. Tanzania kuongea Kiingereza kwenye mahojiano (interviews). Huu ni ulimbukeni ambapo dada zetu hawa na watu wengine wengi wanafikiri wanakuwa kwenye daraja (class/Status) fulani pale waongeapo kiingereza.
Mbona warembo wengine wa nchi ambazo English siyo lugha yao ya taifa huongea lugha zao wanapo hojiwa?
Mi si hungi mkono (not suporting)hata wale wanaoongea Ki ingereza wakati wanapotangaza mashindano hayo. Mi mtanzania na nina ipenda nchi yangu na lugha yangu ya kiswahili na haina maana kama sijui kuongea lugha nyingine.
Pia sikubaliani na Mh. Mbunge kufuta mashindano haya yanayofanyika duniani kote. Yapo mashindano ya Sayansi na Teknolojia kama anataka Tanzania ishiriki basi aanze kuongelea na kusaidia kijenga maabara ya sayansi mashuleni.
Asante.
Mdau.Columbus,OH.

Anonymous said...

weka wazi masharti ya mashindano kuwa mshindi lazima ajuwe kiswahili.unalaumu kipuuzi tu kujuwa kiswahili ilikuwa ni part ya ushindi??? siku nyingine utakuja kupata mshindi anajejuwa kichina peke yake.weka masharti na vigezo vya kujiunge sio tu kupiga domo bila busara

Anonymous said...

Huyu dada nae akomae, akiwa kama muwakilishi wa taifa anawajibika bila kushurutishwa, kuheshimu lugha yake na kuringa na hiyo lugha. Miss Tanzania ni balozi wa Taifa kwa nafasi yake, si lazima afundishwe hilo. Kusoma Uingereza haina maana ya kukidharau kiswahili au kujifanya kuwa amesahau. Kama waliotangulia hapo juu naona ni ulimbukeni usiosadia chochote kwa vijana wetu. Wasanii wote hujaribu sana kuchanganya lugha wanapohojiwa kuonyesha kuwa wameenda chuo au wako juu ki namna fulani. Tumia lugha zote unazozifahamu ki ufasaha pale inapohitajika unapata heshima zaidi. Including you miss Tanzania. Kuwa muwakilishi wa kweli.