ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, December 8, 2013

MISS TANZANIA USA PAGEANT ATEMBELEA DARASA LA KISWAHILI DNV

 Kushoto ni mshindi wa Tanzania USA Pageant Joy Kalemera kutoka New Jersey akisindikizwa na mshiriki mwenzake kwenye mashindano hayo Sham Manka (kulia) wakilakiwa na mmoja ya waratibu wa mamiss hao, Asha Nyang'anyi walipotembelea darasa la kiswahili DMV siku ya Jumamosi December 7, 2013.
 Miss Tanzania USA Pageant Joy Kalemera pamoja na mshiriki mwenzake Sham Manka katika picha ya pamoja na viongozi wa Jumuiya ya Watanzania DMV. Katibu wa Jumuiya Amosi Cherehani (kushoto), makamu wa Rais wa Jumuiya ya Tanzania DMV, Bwn. Raymond, Abraham (wapili toka kushoto) mweka hazina, Genes Malasy (wanne toka kushoto) na Raisi wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Bwn. Iddi Sandaly
 Juu na chini ni Miss Tanzania USA Pageant akiongea na watoto wa darasa la kiswahili DMV alipowatembelea jana Jumamosi College Park Maryland.
 Miss Tanzania USA Joy Kalemera pamoja na mshiriki mwenzake Sham Manka katika picha ya pamoja na watoto wa darasa la kiswahili DMV
 Fundi mitambo na Mpiga kinanda wa watoto wa darasa la kisahili DMV Bryan katika picha

 Miss Tanzania USA Pageant akisalimiana na Afisa Ubalozi na Mhe. January Makamba mara tu alipokutanao nje ya darasa la kiswahili alipokua anajitayarisha kuondoka baada ya kulitembelea darasa hilo. Naibu wa mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mhe, January Makamba nae aliliembela darasa hilo lililopo College Park, Maryland.
 Miss Tanzania USA Pageant katika picha ya pamoja na na Mhe, January Makamba.

2 comments:

Anonymous said...

JAMAA ANATUPIA TUPIA KIDOGO KIDOGO MACHO MACHO JAMANI POLE POLE

Anonymous said...

I wish jumuiya ya Watanzania wangejua talents walizonazo hawa watoto ili kusaidia hili darasa la kiswahili linaloendeshwa katika mazingira magumu. Tuna Watanzania wengi hapa DMV ambao wanaweza kusaidia hili darasa. Hata kutembelea na kufahamu ni kitu gani kinaendelea. Tunashukuru waziri January Makamba kuwatembelea watoto na nadhani alishangaa sana kuwaona hawa watoto wa umri mdogo kabisa wakimbwimbia mwimbo wa Taifa! Tunashukuru kwa msaada wa vitabu ulivyotuahidi kututumia na kufuatilia uwezekanaji wa kupata hadithi za mama na mwana na kutambua jitihada za Uongozi wetu kulidumisha hili darasa la kiswahili kwani kuna nafasi nyingi za kitaaluma hapa Marekani. Hawa ndio watakaokuwa walimu wa Kiswahili wa Kesho kwani Kiswahili kinaenea sana hapa Marekani.