Dar es Salaam. Mkazi mwingine wa Tabata Liwiti, Maulid Sarahani (39) amenaswa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), akidaiwa kumeza zaidi ya kete 83 za dawa za kulevya aina ya Heroie zenye thamani ya zaidi ya Sh70 milioni.
Hivi karibuni Mkazi wa Tabata Kimanga, Mariam Makuwani (29) na Mkazi wa Kinondoni, Hadija Shomari (30) walikamatwa uwanjani hapo wakidaiwa kumeza zaidi ya Kete 123 za dawa za kulevya aina ya heroine.
Mkuwani anadaiwa kutoa kete 67 kwa njia ya haja kubwa, huku Shomari akitoa kete 123.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Polisi cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa alidai Desemba 15 mwaka huu saa 8:00 mchana, Sarahani alikamatwa JNIA akisafiri kwenda nchini China kupitia Hong Kong kwa ndege ya Shirika la Ethiopia.
Nzowa alidai walimtilia shaka mtuhumiwa na baada ya kumhoji, walibaini alikuwa amemeza dawa hizo.
Alidai kete hizo zilitolewa kwa awamu nne kwa njia ya haja kubwa; 23, 22, 29, 10 na kwamba anaendelea kutoa dawa hizo.
“Bado anaendelea kuzitoa kete kwa njia ya haja kubwa, mwanzo zilipatikana kete 73 lakini kwa muda huu ninavyoongea (jana) na wewe zimepatikana zingine 10 na kufikia kete 83,” alidai Nzowa.
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment