ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, December 26, 2013

PPF YAIPATIA MAHAKAMA COMPUTA



Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo, Kimara jijini Dar es Salaam, Jones Mahende (Mwenyetai Nyekundu), akipokea msaada wa Computa mbili alizokabidhiwa jana na Mfuko wa Pensheni wa PPF. Msaada huo ulikabidhiwa na timu ya PPF iliyoongozwa na Meneja Raslimali watu wa mfuko huo, Adolar Duwe (Wapili kushoto) Meneja Uhusiano na Masoko wa PPF, Lulu Mengele (Wakwanza kushoto) na Gedeon Mwashihongo, (Watatu kushoto) 

Mfuko wa Pensheni wa PPF, umeikabidhi Mahakama ya Mwanzo Kimara jijini, computa mbili za mezani ili kurahisisha shughuli za kimahakama.

Akikabidhi msaada huo Jumanne Disemba 24 kwenye viwanja vya mahakama hiyo, Meneja Uajiri wa PPF, Adolar Duwe, alisema, Mfuko msaada huo ni sehemu ya ushiriki wa Mfuko katika kusaidia kusukuma mbele maendeleo ya taifa letu.

Alisema, computa hizo zitarahisisha shughuli za uchapaji wa kumbukumbu na taarifa mbalimbali za kimahakama, lakini pia kutunza kumbukumbu.

Akitoa shukurani baada ya kukabidhiwa msaada huo, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Jones Mahende, aliishukuru PPF, kwa msaada huo ambao ni muhimu katika kipindi hiki cha teknolojia ya computa ambayo inaondoa matumiziya mafaili na karatasi.

“Niwashukuru PPF kwa msaada wenu, kwani msaada huu ni muhimu sana katika shughuli zetu za kimahakama na tuna hakika, shughuli zetu zitakwenda kwa kasi na uhakika” alisema.

Meneja Rasilimali Watu wa Mfukjo wa Pensheni wa PPF, Adolar Duwe, akizungumza kwenye hafla ya kuikabidhi mahakama ya mwanzo Kimara jijini Dares Salaam, computa kwa ajili ya kurahisisha uendeshaji wa shughuli za kimahakama. Hafla hiyo ilifanyika kwenye viwanja vya mahakama hiyo jana

Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Janet Ezekiel (Kushoto), akipeana mikono na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Kimara jijini Dar es Salaam Jones Mahende (K-VIS )

1 comment:

Anonymous said...

Ama kweli Tanzania yetu! Computer mbili mpaka kuweka kwenye mtandao and kufanya hafla!? PPF could even give 10 of them and not even sweat a bit!!Too much kujionyesha for nothing!!