Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki Moon akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwenye ofisi yake iliyopo Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani jana tarehe 24/12/2013.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon akimwonyesha sehemu ya kukaa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa ajili ya kufanya mazungumzo naye.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na mwenyeji wake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon alipomtembelea ofisi kwake jijini New York, Marekani jana 24/12/2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mwenyeji wake,Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon mara baada ya kumaliza mazungumzo yao jijini New York, Marekani 24/12/2013.
Bwana Ban Ki Moon alimwalika Rais Kikwete ambapo viongozi hao wawili walijadili masuala mbalimbali ya kimataifa hususan masuala ya amani na ushiriki wa majeshi ya Tanzania katika kudumisha amani sehemu mbalimbali Afrika na katika nchi nyingine duniani. Tanzania ina majeshi ya kulinda amani katika nchi kadhaa ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Darfur nchini Sudan na Lebanon.
Rais Kikwete yupo jijini New York nchini Marekani ambapo anaendelea vyema na ukaguzi wa kawaida wa afya yake.
(Picha na Freddy Maro / Ikulu)

5 comments:
Why he didn't do his so called medical check up in Dar? I thought he was confident with the products of his work of bringing better health services for all Tanzanians.
Vijimambo sensors delete this like you typically do, but the truth must be told.
Why improve them if the ruling class does not use them. Aka ndugu.
Kwani Mheshimiwa Raisi hana DOCTOR hapa Tanzania? Na kama yupo analipwa kumcheki nini? Just asking!
Mdau hapo juu umemlipia nauli? Mbona kila kukicha tunasikia watu wameenda India. Mkuu wa nchi huyo ana connection nyingi labda kaambiwa njoo we will take care of everything.
Mdau wa 4 acha uvivu wa kufikiria. His bills are paid by us "we the people of United Republic of Tanzania". Safari za rais siyo safari zako za kwenda India. Rais anamsafara. Nani atawalipia hao watu wote na kwanini? Huyo mlipaji anategemea nini in return?
Post a Comment