ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, December 10, 2013

USALITI HAUNA NGUVU, SHETANI WA USALITI NI AKILI ILIYOKOSA MALENGO-2


Mada hii ikujenge kutambua kwamba hakuna kilicho na nguvu kuliko akili yako. Wiki iliyopita niligusia kuhusu mke kuwa amelala kisha anamruhusu mume wake aende chumbani kwa dada yake (iwe mkubwa au mdogo), wanachozungumza huko hakijui. Baadaye anapokuja kubaini kwamba kati yao kuna uhusiano usiofaa, anabaki kulia kwa kusaga meno, majuto na masikitiko. Majuto ni mjukuu!

Yupo mwanamke ambaye mwanzoni alikuwa akimchukia mwanaume fulani. Walipoanza kuwa karibukaribu, historia ikabadilika. Pale huwezi kuthubutu kutamka kwamba kilichowafanya wawe wapenzi ni nguvu ya usaliti, isipokuwa ni udhaifu wa nyoyo zao.
Msomaji wangu Lauryin Joe (siyo jina lake halisi), alinisimulia kisa chake cha kutoka kimapenzi na kijana mpangaji mwenzake, mumewe akajua na kusababisha uhasama mkubwa. Anasema: “Mwanazoni sikuwa na wazo kabisa, nilijiamini mimi ni mwanamke imara katika ndoa yangu.

“Tuliishi kwenye nyumba moja na kijana anayeitwa Paul, yeye hakuwa ameoa. Tukaamua kuishi kama familia moja kwa upendo kabisa. Maisha yalikuwa na maelewano kabisa, huku tukichangia kila kitu. Paul alitambulika kama mdogo halisi wa mume wangu.
“Tatizo kubwa ambalo mpaka leo nalijutia ni utani kati yangu na Paul. Kadiri maisha yetu yalivyokuwa yanakwenda mbele, ndivyo na mazoea yalivyoongezeka. Mimi na Paul tulitaniana sana. Utani ulikuwa mbaya zaidi pale tulipoanza tabia ya kuvutanavutana na kushikanashikana.

“Kuna wakati Paul alikuwa amekaa, mimi nilimnyatia kwa nyuma na kumfumba macho ili abahatishe ni nani. Naye badala ya kunitaja moja kwa moja, alianza kwa kunishikashika maeneo tofauti, mimi wala sikumkataza. Alinishika makalioni, niliona sawa tu.
“Mazoea yaliongezeka, nyakati nyingine asubuhi, nikiwa nimetoka kuamka, huku nikiwa na kanga moja tu, nilimfuata Paul na kumkumbatia. Kumbe joto langu likawa linaongeza kitu kizito chenye nguvu kubwa ndani yake, vilevile kwa upande wangu, mwili wangu uliakisi msisimko wa ajabu kila nilipomkumbatia.

“Paul alikuwa kijana anayejishughulisha na ukinyozi wa saluni, mimi ni mama tu wa nyumbani. Kutokana na namna tulivyozoeana, hata utendaji kazi wa Paul ulipungua, maana wakati mwingine alishindwa kwenda kazini, mimi na yeye tukabaki tu nyumbani, tunazungumza na kucheza michezo ya aina mbalimbali.”

HATUA IKAWA MBAYA ZAIDI
Lauryin anasema: “Kuna kipindi Paul alianza kusumbuliwa na ugonjwa ngozi (mba), alishambuliwa zaidi usoni, mgongoni na kifuani. Hakunificha kitu, aliponunua dawa ya kupaka, aliniambia, ikabidi niwe namsaidia kumpaka maeneo ambayo yeye hawezi kuyafikia.
“Vilevile nami nikuwa na mba kidogo kifuani, kwa hiyo kila siku jioni na asubuhi, kila mmoja alioga, kisha nilikwenda chumbani kwake, alivaa bukta tu ili kuruhusu nimpake dawa maeneo yote. Mimi nilikuwa nimevaa kanga moja, mtindo wa ‘passport size’, kuwezesha naye anipake dawa kwa urahisi.
“Hapa naomba nikiri kwamba pamoja na makosa yangu na Paul kama wasailini lakini ukweli utabaki kusimama kwenye eneo lake kuwa mume wangu ni mkosaji kwa sababu hakuwahi kunionya ukaribu wangu na Paul, alitupa uhuru. Itaendelea.
Mimi nilikaa sebuleni na Paul tunaangalia TV peke yetu, yeye akiwa amelala chumbani.”

Itaendelea wiki ijayo.

GPL

No comments: