ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, January 8, 2014

BAADA YA NUMBER ONE REMIX NA DAVIDO MOVIE INAENDELEA SASA NA HUYU NDIYO NEXT

DIAMOND 

Bombshell ya remix ya My Number One aliyomshirikisha Davido haimtoshi Diamond Platnumz kwakuwa bado anatarajia kudondosha nyingine. Tayari ameshafanya collabo na Iyanya huku akiipigia hesabu pia collabo nyingine na hitmaker wa ‘Nwa Baby, Mr Flavour.Akizungumza na Capital FM jijini Dar es Salaam, Diamond amesema safari ya Nigeria imempa connection nyingi.
MR. FLAVOUR
“Nigeria wanaitaka marker ya East Africa,” amesema Diamond ambaye video ya remix ya ‘My Number One’ imeangaliwa kwa zaidi ya 100,000 hadi sasa. “Kuna connection nyingi nimezipata nikiwa Nigeria nimefanya ngoma na Iyanya bado haijatoka itatoka baadaye. Pia nilikuwa naye amenisupport vitu vingi hata wakati na kurelease ngoma kwenye Youtube kwenye nini, amekuwa anatweet amekuwa annapost ili kuipa kiki ngoma yangu. Watu tofauti tofauti nimekutana nao ili kuangalia tufanyaje kazi pamoja,kwabababu wao ndio wameshika muziki wa Afrika kwa sasa hivi. Pia Mr flavor nina project naye.”

No comments: