ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, January 5, 2014

CHAMA CHA MAPINDUZI DMV




Tumepokea kwa mshituko mkubwa na majonzi makubwa habari za kifo cha BI ZAINABU BUZOHELA DULLAH Marehemu 
alikuwa mcheshi mwenye heshima kwa mkubwa na mdogo yuko karibu na kila mtu yuko mstari wa mbele kwa kila jambo ameacha pengo kubwa si kwa familia yake bali kwa watanzania wote tunaoishi hapa DMV na Marekani kote kwa ujumla amefarki ukiwa mchango wake unahitajika Tunatoa pole sana kwa mama wa marehemu [Da Rehema] jana tulipata nafasi ya kumfariji na tukamuomba kuwa no moyo wa subra katika kipindi hiki kigumu Tunatoa pole sana kwa mume wa marehemu bw DULLAH tunakuomba uwe na moyo wa subra na kumshuru Mwenyeenzi MUNGU Tunatoa pole kwa ndugu jamaa na watanzania wote TUNATOA WITO WA MICHANGO STATE ZOTE NA DUNIANI KOTE KUCHANGIA KWA HALI NA MALI KUFANIKISHA KUSAFIRISHA MWILI WA MAREHEMU NYUMBANI TUNAMUOMBA MWENYEENZI MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI AMEN


1 comment:

Anonymous said...

UCCM katika misiba? kwani Utanzania hautoshi? au ndio mambo ya kutengana kwa itikadi?