Jamani Ivi ni nani kwenye USO huu wa dunia ambaye ajawai kukosea??????
Wapo binadamu wenzentu wanamakosa makuubwa Na hatuyajui na mengine yanajulikana....
Kwanini tumekuwa mstali wa mbele kuwanyooshea watu vidole pale wanapokosea Tena Na kuwaombea Mabaya....... Dah!
Tukumbuke Sisi sote ni binadamu akuna anaejua kesho yake
Sina maana tutete uovu au kosa linapoafanyika Bali tutumie muda kutafakari kabla ya kumuhumu MTU
Wanawake wenzangu huyu ni Mwanamke mwenzetu lakini sisi ndio tumekuwa mstari wa mbele kumlaani Na kutolea maneno mashafu Na hali Yukuwa tunajua hakuna alie mkamilifu
Binafsi imeniuma Na nimejiskia vibaya sana
SAWA KAFANYA KOSA
Ila tusiwe majaji wa kutoa hukumu anza kujihukumu kwa maovu yako kabla ya kumuhukumu mwenzako
Tafakari maovu yako kabla kumnyooshea kidole mwenzako
TUACHE MAMLAKA ZA SHERIA ZIFANYE KAZI YAKE
Wanawake wenzangu TUPENDANE Natuwe na umoja Tushilikiane na tushauliana katika maamuzi yetu madogo Na makubwa labda tutaepuka ili tatizo
Inawezekana haya yote yanatokea kwetu sisi kwa kukosa ushilikiano Na upendo
JACK DADA ANGU UMEKOSEA
Ila Sina sababu ya kukulaumu au kukuhukumu
wakati mwingine binaadamu ujifunza katokana Na makosa mungu ni wetu sote inshaallah atakusimamia.
Nimeshidwa kuvumilia nimeamua kusema nilichosema ila kama Kuna nilie mkwaza
naomba Aniwie radhi.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU TUBARIKI WATANZANIA
By Dayna nyange

8 comments:
The mdudu,,anasema kwani huyu dayna ni nani hasa? Atetee mambo ya kijinga yanayo haribu taifa la leo na kesho kwanza ajiangalie mwenyewe kwajinsi alivyokosea na anavyozidi kukosea kila kukicha na nyimbo zake za kukopy na kupest nyimbo mwanzo mpaka mwisho madudu matupu pasipo na ujumbe wa maana kwenye jamii yetu ya wana Morogoro na tanzania nzima,mm natoka moro kama ww lakini kamwe sikufagilii hata kidogo,watu wetu wenye ujumbe ni Afande Sele?,Stamina n Mc koba
kwani na wewe c ndo haohao, bd kukamatwa tuu, siku yako inakuja,nakwambia ungekuwa na ndugu zako walioathiarika na hayo madawa wala usingeandika huo upumbavu, tena unyamaze uache kujishaua.
Dada uliyeamua kujitoa muhanga kuzungumzia hili, ushukuriwe umeamua kusema yaliyoko moyoni mwako, tusihukumu wanawake ila unapo zaa mtoto unatarajia afanye mema.... na mwanao akianza kula unga mzazi unapoteza mwelekeo, na hata kama umemwandalia mazuri yote yanapotea
Sasa iweje wewe na akili zako umteteeee mtu ambaye kwannza anajiua mwenyewe kwa kubeba madawa yote hayo, na kuamua kuyapeleka sehemu kwa ajili ya kuharibu maendeleo ya watu na maisha yao. Hivi huyu ikiwa aliweka ahadi zake na hazitimizwi, we kweli una akili au ni wale wale (usi hukumu, nyamaza kimya na umuombe Mungu)
Dada ulichosema ni kweli, walio wengi wamesahau kua kule kubeba tu huo mzigo ni adhabu ya mwili wake, nataka kukuhakikishia walio wengi wanao msema huyu dada ndio wazinZi walioshindikana, na for the most part ni wivu. Inasikitisha kuona walio wengi wanamwombea anyongwe, hiyo inaonyesha jinsi gani wanadamu wanaweza kukua muda wowote wakukupatia nafasi. Hivi kwanini umuombee mtu mwingine kunyongwa na mchina wakati serikali ya Tanzania imewaruhusu wachina na biashara zao fake tele Tanzania, inaonyesha jinsi watz tuna ufinyu wa kufikiri. Simjui huyu dada isipokua nimemwonea huruma maana naamini amejitumbukiza humo alimo kwa kua shetani sasa hivi ndie anatawala dunia. Jamani ndugu zetu tujaribu kujifunza kutonyooshea wenzetu vidole bali tuombeane.
Eti na yeye ametoa maoni yake huyu?. Hizi ndio akili za kufikiria kila jambo Kibongo bongo tu. Watu wamekosa maono na wala hawajitambui tena. Hivi ameshindwa kitambua 'jinai' mbaya kabisa inayomkabili huyo msichana mwenzie?
Tumekuwa taifa la watu hovyo, tunajaribu kutetea hata visivyo tetewa katika macho ya kimataifa.
Wewe Diana Nyange nakuomba sana ukae Kimya! Kwani akiwa msichana mwenzetu ndo tukubaliane na makosa yake?? Kubeba unga/sembe nikosa hilo halibadilikii hata kidogo! Biashara za kufanya zipo nyingiiii sana sana sana kwanini hiyo haramu ndo wasichana wengi wana ng'ang'ania tu?? Kwanini? Kwasababu Ni wavivu hawataki kufanya kazi wanataka kuishi maisha ya juu wasio ya muduu na hiyo Ni dhambi kubwa sana!! Kwahiyo unachotetea hapaaa hakina mshiko kabisaaa! Wasichana wajifunze kuwajibika na sio kuwa mapunda/wabebaji sembe/unga/drugs. Mungu ibariki Tanzania...
Mtoa mada anahitaji usimamizi tena thabiti anapoamua kupost chochote kwani uwezo na upeo wake unaonekana kuwa chini sana la sivyo naye atanyongwa siku za karibuni. Ameshindwa kutofautisha baina ya kukosa na kukosea.
Muathirika amekosa kwa sababu suala la kuuza, kutumia au kusafirisha madawa ya kulevya analijua fika kuwa ni jinai na lina madhara makubwa sio kwa taifa tu kwa ujumla bali kwa yeye na ndugu zake pia.
Huku akiwa anajua hivyo, akaamua akiwa na akili timamu kufanya jambo hilo kwa ukatili, kiburi na ubabe mkubwa. Mtu anayekosea ni yule ambaye ameteleza, amefanya jambo bila kujua kuwa ni kosa, japo kutojua kuwa ni kosa hakumuweki pahala salama, lakini anawezapata huruma ya umma (ambayo haitamsaidia pia).
Mimi naomba sana sheria za China zichukue mkondo wake kama ni kifungo au kunyongwa mpaka hapo uongozi wa Tanzania utakapoona raia wake wanapukutishwa ndio wataamka. Anayesema kuwa wanaomlaumu ni wifu tunasubiri arobaini zake ataingia tu naye. Pumbafu sana mtoa mada
Akihukumiwa duniani kwa hukumu kali gerezani pengine ataupata msamaha Mungu mbinguni na kuiona pepo na kama hatohukumiwa duniani atapata adhabu ya Mungu huko mbinguni Jehanam...sasa kama unampenda huyu dada apate hukumu wapi wandugu?
Post a Comment