“Umemwona Wema, kwa sasa ana ngozi nzuri yenye afya na iliyo na mng’aro kama alivyokuwa awali,ni nzuri sana yani, ameacha kabisa kutumia dawa za kung’arisha ngozi hilo ndilo lililonivutia zaidi kwani alisikiliza ushauri niliompa kabla.”
Hiyo ni kauli ya staa aliyetikisa mwaka 2013 bwana Diamond Platnumz aliyoitoa hivi karibuni alipokuwa akizungumza na gazeti maarufu la michezo nchini hivi karibuni.
Diamond amesema Wema ndiye mwanamke anayetamani kuwa naye katika maisha yake, hivyo kauli yake aliyoitoa mwanzo kuhusu kuzaa na Wema ipo mbioni kutimia.
“Miezi kadhaa nyuma niliongea kuhusu nia yangu ya kuzaa na Wema, wakati huo nilikuwa bado na Penny, siwezi kukimbia kivuli changu kwani ukweli unabaki palepale nampenda yule binti, japokuwa wapo wanaosema kwamba sijatulia au natafuta ‘kiki’ kupitia warembo hawa, si kweli, Wema nilikuwa naye kabla ya Penny na vigezo vyangu ni mchumba anayejali kazi yangu na kujua kwamba mimi ni staa nahitajika sehemu yoyote, muda wowote, Wema ni mwelewa.” Alisisitiza Diamond

4 comments:
DJ Luka....hakuna mtu mwenye shida na Diamond au wema. Kama huna cha kupost basi walau zungumzia namna watu wanavyoweza kuondokana na umaskini....Asante Dj Luke
Ebu na wewe ..dogo Dimond kua basi kidogo hawa wanawake itafika kipindi watakudharau..kubwa mfano mzuri kwa watoto au vijana wanakuona wewe ni mfano..Pesa na jina sio kila kitu...tulia na mdada wa watu..unamchezea wa nini au kwa sababu unajua anakupenda..then stop it using her
Hakuna mume kama daimond kwa wema na hakuna mke kama wema kwa daimond oaneni basi mnaenda tabia zenu u are crazy for each other.
we unaempangia bloga what to do..fungua yako tukuchambe kama mwanafulani.. hutaki kusikia ya wema...pita kimya kimya...
diamond n wema kama chriss na rihana... wote waluwalu
Post a Comment