Waumini wa kanisa la Orthodox nchini Ethiopia wakishiriki katika sherehe ya mwaka ya sikukuu inayofahamika kama Timket katika mji wa Addis Ababa Jumamosi iliyopita. Sherehe hiyo ni ya kukumbuka ubatizo wa Yesu Kristo mto Jordan na Yohanne mbatizaji kulingana na Imani ya kanisa hilo.
Waumini wanyunyiziwa maji ya ubatizo katika sherehe hizo
Katika siku hiyo nchini Afrika kusini,mfuasi wa Kihindu aliyetoboa mashavu na kifua alitembea toka mwanzo hadi mwisho wa mji wa Durban wa Chartsworth
Mamia washiriki katika sherehehiyo ambapo watu hupitia matambiko machungu kama ishara ya Imani na toba kwa heshima ya Mtukufu Mariga.
Waendeshaji baiskeli washindana katika hatua ya saba na ya mwisho ya Tour du Gabon jijini Libreville.Mbelgiji Fredrique Robert ndiye aliyeshinda hatua hiyo naye Natnael Berhane wa Eritrea ndiye aliyeshinda hatua zote za mashindano hayo.
Alhamisi:Mwanaume kutoka Misri akisafiri kwenye Punda kando ya gwaride la heshima kwenye barabara inayoelekea kwenye mazishi ya polisi waliouawa baada ya wapiganaji kuwafyatulia risasi katika kizuizi cha polisi wilayani El-wassta katika mkoa wa Bani Suief,kusini mwa Cairo.
Siku mbili awali,Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe akishika Rosari alipohudhuria mazishi ya dadake Bridget katika mji wa Zvimba,magharibi mwa Harare.Mugabe atakayeadhimisha miaka tisini tangu kuzaliwa kwake mwezi ujao,ameishi zaidi ya nduguze watano.
Maharamia washukiwa wa Somalia waliokamatwa na jeshi la wanamaji la Kiholanzi waonekana gerezani katika mji wa Mombasa nchini Kenya.Wanaume hao walikabidhiwa mamlaka ya Kenya kwa kuwa Somalia haijakuwa na mfumo wa Sheria kwa muda wa miongo miwili sasa.
1 comment:
MBONA HAWA HAWAITWI AL KAIDA SI WANA MSIMAMA MKALI NA DINI ZAO AU NDO DOUBLE STANDARD KWA WENGINEWE WAKIWA WANAABUDU MARA HUSINGIZIWA HAOO MAGAIDI LAKINI WENGINEW WAKIABUDU KWA IMANI ZAO WAA KWAO POA
Post a Comment