Katika mahojiano ‘spesho’ na gazeti hili yaliyofanyika kwenye ofisi za Global Publishers, Bamaga, Mwenge, Dar es Salaam, juzi, Masogange aliamua kumwanika kigogo huyo huku akimtaja jina bila kuuma maneno.
Melisa Edward.
TWENDE PAMOJA Risasi: Masogange tumekuita leo hapa kwa ajili ya mahojiano maalum. Tangu umerudi Bongo toka Afrika Kusini ulikokutwa na ule msala wako, naamini hujawahi kuzungumza na chombo chochote cha habari. Uongo, kweli?Masogange: Kweli kabisa.
Risasi: Risasi linakukaribisha tuzungumze mambo muhimu, lakini kubwa kuliko yote, hebu mtaje mtu aliyekutuma kubeba ule unga ambao ulikamatwa nao Afrika Kusini.
Masogange: (akionesha sura ya umakini) kusema ule ukweli, ni…(anamtaja jina). Huyu bwana ndiye aliyeniponza kwa yote yale.
Risasi: (bila mshtuko baada ya kutajwa kwa jina hilo). Huyo mtu ni Mtanzania kweli?
Masogange: Hapana, ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ila anaishi Tanzania miaka nenda, miaka rudi.
Risasi: Sasa Masogange, huyu mtu ilikuwajekuwaje hadi akakutuma kupeleka mzigo ule Afrika Kusini, hapo pana utata kidogo.
Masogange: Wengi hawajui. Iko hivi, siku ile (Julai 5, 2013) mimi nilikuwa nasafiri kwenda Sauz kwa mambo yangu tu. Nilipofika pale Uwanja wa Ndege (Julius Nyerere International Airpot) nilimkuta huyo mtu.
Risasi: Naye akiwa anasafiri kwenda huko?
Masogange: Hapana. Yeye tunafahamiana kwa muda mrefu, aliponiona aliniuliza kama nakwenda Sauz, nikamwambia ndiyo. Akasema anaomba nimbebee mizigo yake ya sukari.
Nilimkatalia, lakini akasema kuna mtu atanipokea Uwanja wa Ndege (wa Kimataifa wa Oliver Tambo) uliopo (Kempton Park) Johannesburg.
Basi nilimkubalia, lakini…
Risasi: Subiri kwanza Masogange. Hapo una maana wewe kazi yako ilikuwa kubeba tu, baada ya kutua kule ungekutana na mwenye mzigo, Je, uliuangalia mzigo wenyewe kama kweli ni sukari?
Masogange: Ndiyo. Nilimwambia anifungulie nione kama kweli ni sukari, akafungua begi moja, nikachungulia na kuona kweli ni sukari nyeupe!
Nilimwambia kama anataka nimsaidie kuufikisha Afrika Kusini, apeleke mpaka kwenye ndege ili kunipunguzia kazi ya kubebabeba. Nikifika Sauz nitamtolea huyo mtu sukari yake.
Basi, akapeleka mpaka kwenye ndege, mimi nikapanda na safari ikaanza.
Risasi: Subiri kidogo Masogange. Wewe ulikamatwa na mtu anayedaiwa ni ndugu yako, Melisa Edward. Mbona humtaji?
Masogange: Oke, yule tulikuwa safari moja tu. Lakini yule Mkongomani anajuana na mimi.
Risasi: Oke, endelea.
Masogange: Tulifika uwanja wa ndege salama. Nikashuka na yale mabegi nayo, lakini cha ajabu wakatokea askari na kutukamata.
Waliniuliza nimebeba nini? Nikawaambia sukari, wakasema siyo sukari, wakanitaka nilambe. Kulamba hivi, ndiyo nikajua kweli siyo sukari, tukawekwa chini ya ulinzi na kupelekwa kwenye vyombo vyao vya sheria kwa hatua zaidi.
Risasi: Pole sana. Kwa hiyo yule mtu ambaye angepokea mzigo kule Sauz ulimwona ulipotua uwanjwa wa ndege?
Masogange: Sikuwa namjua kwa sura, nilipewa mawasiliano yake tu. Kuna uwezekano alituona wakati tumekamatwa na polisi maana tulizungukwa na watu wengi.
Risasi: Unakumbuka yalikuwa mabegi mangapi ya hiyo ‘sukari’?
ANAYEMJUA MWAKYEMBE
Siku chache baada ya mlimbwende huyo kunaswa Sauz, Bongo, Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison George Mwakyembe alimtaja kijana ajulikanaye kwa jina moja la Mangunga kwamba ndiye aliyedaiwa kuwa na video queen huyo ndani ya ndege kwenda Afrika Kusini.
Kamanda Nzoa aliwataja wanawake hao baada ya kukamatwa kuwa ni Agnes Jerald ambaye alisema hajapiga hesabu ya umri wao, ila alizaliwa mwaka 1988 na Melisa Edward ambaye alisema amezaliwa mwaka 1989.
Mwakyembe aliamuru kijana huyo asakwe na kukamatwa ili kujibu mashitaka ya kusafirisha madawa ya kulevya aina ya Methamphetamine kwa Tanzania huku Sauz ikisema ‘unga’ huo ni ephedrine ambao si wa kulevywa bali ni malighafi haramu.
Nassoro.
Masogange na mwezake, Melisa walikamatwa Julai 5, mwaka jana kwenye uwanja huo wa ndege nchini humo wakiwa na madawa hayo yaliyokadiriwa kuwa na thamani ya shilingi bilioni 6.8.Kesi yake iliendeshwa na Mahakama Kuu ya Gauteng iliyopo Kempton Park nchini humo na alikutwa na hatia ambapo alihukumiwa kwenda jela miezi 32 au kulipa faini ya randi 30,000 (shilingi milioni 4.8). Masogange alilipa faini huku mwenzake, Melisa akiachiwa huru kukutwa hana hatia.
GPL
8 comments:
Anayeamini hii hadithi namuonea huruma, mchanga wa macho huu.
NINAMSIFU HUYU BINTI KWA KUMTAJA HUYO KIGOGO, NATUMAINI SERIKALI ITAMSHUGHULIKIA HUYO KIGOGO BILA YA AIBU. WAKATI MWINGINE INABIDI KWENYE KESI KAMA HIZI KUCHACHAMAA NA KUONYESHA MFANO KWA WATAKAOFUATIA KUTUMA WATOTO WA WATU KUBEBA MADAWA. KAMA ILIVYOANDIKWA HAPA NI KWELI HUYU BINTI ILIKUWA ASILIPWE HATA SENTI TANO KWA UPUNDA HUU.
TUKIRUDI NYUMA JAMANI MSIPENDE KUBEBA MIZIGO YA WATU ESPECIALLY KAMA MNAJUANA JUU JUU.
muwongo mkubwa huyu mdada anawajua vizuri walio mtuma anaficha siri zao amepewa msiko hatari sana utakao msaidia maishani hatokuwa maskini daima muongo bwana eti mkongomani nilicheka sana nilivyo soma hii habari hakuna ukweli wowote vigongo wa juu wanajulikana ndo waliomtuma na wala si mkongomani awadanganye hao hao lakini si sisi
Watanzania sio wajinga ku buy this no sense story.Na kama story hii ndio kama ilivyo basi dada huyu kichwani ni mtupu kabisa.tangu lini mtu asafirishe sukari nje ya nchi kwenye bagi?na unatoa sukari Tz unapeleka south Africa? Ni km kutoa maji kwenye bahari kuweka kwenye bwawa!!! Story hizi za kubeba vyakula nikwenye 'igembensabo' bus service kwenda vijijini.
This story is nonsense!!! Anachekesha walio nuna-tafDhali sana asitudanganye sie sio wapumbavu hata kidogo! Utatoaje sukari TZ upeleke SA? Tena kwenye ma begi ya nguo? Huyu dada Ni bora tu afunge mdomo wake kabisaaa tena akae kimyaaaaa!! Asiongee tena! Hiviii Watanzania lini tumekuwa wapumbavu na wagonywa wa Aakili jamani? Lini? Huyu dada anataka kutufanya sie vichaaaaa? Hakuna anayeaaamini hii story hata kidogo, hata chembe. Story tunaijjua kuwa huyo Kigogo yupo hapa hapa nchini na nimtanzania mwenzetu Hivyoo hakuna cha mkongolizi wala Mjamaika wala Mnaigeria na wala msomali! Tafadhali akae kimyaaaa kabisaaa. Mungu ibariki Tanzania.
Huyu dada na hao waandishi waliomuhoji na kuiandika hii story wote wajinga na watupu kichwani.
1. Huyo mkongomani kama alikuwa hasafiri yeye ilikuwaje azibebe hizo Sukari mpaka kwenye ndege? So walimrusu hapo airport sio? Maana hivyo ndivyo anavyosema huyo Masigonge kuwa alimwambia azibebe mpaka kwenye ndege ili yeye "Masigonge" asipate shida ya kubeba beba huo mzigo?
2. Hayo mabegi tumeambiwa yalikuwa mengi na pia yalikuwa CHECKED-IN sio kana kwamba ni carry-on, so now story anayotupa yeye na hao waandishi wajinga kuwa yalibebwa mpaka kwenye ndege, SERIOUS???
Mi nawalaumu hao waandishi wa bongo, thay are good kuandika na kuchunguza umbra ambao hauna faida but kwenye habari muhimu vichwa vyao ni maji matupu!!!
Huyu dada na hao waandishi waliomuhoji na kuiandika hii story wote wajinga na watupu kichwani.
1. Huyo mkongomani kama alikuwa hasafiri yeye ilikuwaje azibebe hizo Sukari mpaka kwenye ndege? So walimrusu hapo airport sio? Maana hivyo ndivyo anavyosema huyo Masigonge kuwa alimwambia azibebe mpaka kwenye ndege ili yeye "Masigonge" asipate shida ya kubeba beba huo mzigo?
2. Hayo mabegi tumeambiwa yalikuwa mengi na pia yalikuwa CHECKED-IN sio kana kwamba ni carry-on, so now story anayotupa yeye na hao waandishi wajinga kuwa yalibebwa mpaka kwenye ndege, SERIOUS???
Mi nawalaumu hao waandishi wa bongo, thay are good kuandika na kuchunguza umbra ambao hauna faida but kwenye habari muhimu vichwa vyao ni maji matupu!!!
huyu nay Agnes anaona waaaatu wajinga ,,kweli unatoa story kama hiyo?haina mbele wala nyuma,,,hata mtoto wa miaka kumi anaona ni hadithi hadithi..acha kufanya interview kaa kimya ,,story za kitoto acha
Post a Comment